Na Israel Mwaisaka, Timesmajira Online,Rukwa
Jeshi la Polisi mkoani Rukwa linawatafuta watu wanaodaiwa kuhusika kufukua kaburi la Julius Ladislaus (24) aliyefariki Novemba 2024 na kuondoka na mwili wa marehemu.
Akizungumza na waandishi wa habari Kamanda wa Polisi mkoa wa Rukwa Shadrack Masija,amesema Julius alifariki Novemba 2014 wilayani Chunya mkoani Mbeya na mwili wa marehemu huyo kusafirishwa mkoani Rukwa na kuzikwa Kijiji cha Lunyala wilayani Nkasi.
Masija amesema, Februari 14,2025 mwili wa marehemu ulikutwa umefukuliwa na kuchukuliwa na huku sanduku na kaburi lake vikiwa wazi.
Hivyo amewaomba wananchi kutoa taarifa ili Watuhumiwa waliofanya tukio hilo waweze kukamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.
Huku akisisitiza kuwa jeshi hilo linaendelea na uchunguzi juu ya suala hilo,ambapo amedai tukio hilo linahusishwa na imani za kishirikina,hivyo amewasihi Wananchi kuachanq na imani hizo ambazo kwa kipindi hiki zimepitwa na wakati.
Sambamba na hilo pia jeshi hilo linamtafuta mtu mmoja ambaye hadi sasa hajajulikana kwa tuhuma za kuhusika na kifo cha mwanamke mmoja aliyekutwa amefariki katika nyumba ya kulala wageni mjini Namanyere.
Alidai kuwa mnamo Februari 19,2025 binti huyo mwenye umri wa miaka 19 akiwa na mwanaume ambaye bado hajajulikana alikutwa amekufa katika nyumba ya kulala wageni.Baada ya kifo cha mwanamke huyo kijana huyo wa kiume alikimbia na hadi sasa hajulikani alipo.
More Stories
Mipango 10 kabambe ya TPA
Bilioni 15 kukopeshwa wanawake,vijana jijini Dar
Serikali yaendelea kubuni mbinu kukabiliana na wanyamapori wakali