Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online
WANANCHI wametakiwa kuunga mkono juhudi za serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hasa katika utekelezaji wake wa miundombinu mbalimbali ikiwemo ujenzi wa viwanja vya ndege, kuleta wawekezaji lakini pia ununuzi wa ndege za abiria na mizigo .
Rai hiyo imetolewa jana Julai 7, 2023 jijini Dar es Salaam na Katibu mtendaji wa Baraza la Ushauri la Watumiaji Huduma za Anga(TCAA-CCC),Innocent Kyara wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kwenye Bando lao kwenye maonesho ya 47 ya kimataifa ya biashara maarufu sabasaba yanayoendelea.
“Tunaaipongeza serikali juu ya jitihada mbalimbali ambazo wamekuwa wakifanya, imekuwa ikijitahidi kuifungua nchi yetu, kutafuta wawekezaji, fedha kwaajili ya miradi mbalimbali hivyo ni jukumu letu kama wananchi kuunga mkono”
“Hivi karibuni shirika la ndege Tanzania ATCL ilileta ndege ya mizigo ilipaswa Kila Mtanzania macho na masikuo yake awese kujielekeza kuangalia namna gani atafaidika na Ile ndege” Alisema Kyara na kuongeza
“Tunafahamu serikali inajenga miundombinu mbalimbali ya viwanja vya ndege, hivyo tuache kuibeza miradi hii, kubeza wawekezaji wanaokuja na fursa nyingi ambazo Kila mmoja wetu anaweza akafaidika nazo”.
Hata hivyo,Kyara amewataka watanzania wanaotumia usafiri anga kuhakikisha wanafuata kanuni na taratibu zilizowekwa wakati wanapotumia usafiri huo ili kujiepusha na kadhia.Kadhalika,Kyara amewataka watanzania kujitokeza kwenye banda lao la TCAA-CCC kujipatia elimu .
“Tupo ndani ya maonesho haya kwa miaka 17 sasa kubwa ikiwa ni utekelezaji wa majukumu yetu lengo ni kutetea wafanyabiashara”Amesema Kyara.
Naye, Kennedy Walter ambaye ni mwanafunzi,amewahimiza kujitokeza kwenye Banda la Baraza la ushauri la watumiaji Huduma za Anga (TCAA(CC))kwa ajili ya kujipatia elimu.
More Stories
Mpango ashiriki mazishi ya Mama yake Serukamba
TRA kuongeza idadi ya waendesha uchumi walioidhinishwa
TRA Tanga wajivunia ukusanyaji mapato