Na Esther Macha Timesmajira Online , Chunya
Wananchi mkoani Mbeya wametakiwa kuunga mkono juhudi za Rais Samia za kupambana na uharibifu wa mazingira kwa kuzuia ukataji miti ovyo pamoja na kulinda vyanzo vya maji.
Hayo yameelezwa na Mbunge wa Vitimaalum Mkoa wa Mbeya ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maji Mhandisi Maryprisca Mahundi katika tamasha la Maryprisca Mama Ntilie Festival 2023 lilofanyika Mamlaka ya Mji Mdogo Mbalizi ikiwa ni halmashauri ya tano kufikiwa na fursa ya kuwawezesha wanawake kiuchumi kwa kuwapa mitaji,mchele,fedha na majiko ili kuongeza mitaji kwenye biashara zao.
Mahundi amesema Rais Dkt. Samia anafanya kazi kubwa ya kulinda mazingira hivyo wananchi wamuunge mkono pia anafanikisha miradi ya miundombinu,elimu,afya na uchumi kwa kutoa mikopo katika halmashauri.
Amesema lengo la kuandaa tamasha hilo ni kuwaunganisha wanawake kupendana na kuhakikisha wanajikwamua kiuchumi ili familia ziwe bora na kukataa ugolikipa hivyo wafanye kazi kwa bidii na wasiidharau kazi ya Mama Ntilie.
Wanawake zaidi ya 100 wameshiriki katika tamasha la Mama Ntilie Festival 2023 Wilaya ya Mbeya na wote wamekabidhiwa mitungi ya gesi kutoka kampuni ya Oryx na litaendelea katika Halmashauri ya Jiji la Mbeya na kuhitimishwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali.
Lawena Nsonda (Baba mzazi) ni mdau wa .aendeleo katika wilaya hiyo amesema kuwa Mbunge huyo anafanya kazi kubwa hususani katika suala zima la kulinda mazingira.
Diwani Vitimaalum Kata ya Makongolosi wilayani Chunya, Sophia Mwanauta amesema kuwa kitendo kinachofanywa na Mbunge huyo ni mfano tosha kuwa anawajali wanawake wa hali ya chini.
More Stories
TASHICO,yatoa ufafanuzi Mv.Serengeti kutitia upande mmoja
TAG yampongeza Rais Samia
CCM Tabora yamfariji mjane wa kada anayedaiwa kujiua