Na Judith Ferdinand, TimesMajira Online, Mwanza
Imeelezwa kuwa changamoto ya ugonjwa wa corona,bado ipo hivyo wito umetolewa kwa wananchi wa Mwanza kuhakikisha wanapata chanjo ya Uviko-19.
Wito huo umetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Robert Gabriel,wakati akizungumza kwenye hafla ya upokeaji wa vifaa tiba na upanuzi wa jengo wagonjwa mahututi (ICU) katika hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando kupitia fedha za Uviko-19,ilifanyika Julai 5,2022 hospitalini hapo jijini Mwanza.
Mhandisi Gabriel, ameeleza kuwa chanjo hiyo inasaidia kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa wataalamu wa afya kwa mtu ambaye amechanjwa chanjo hiyo ya uviko-19 kinga inaimarika na changamoto za Uviko-19 duniani bado hazijaondoka.
Hivyo amewaomba wanamwanza wenzake wahakikishe kwamba wanapata chanjo hiyo,wale waliochanja wanapopata mashambulio ya uviko-19 kinga inakuwa imeimarika na wanapata maudhi madogo madogo na afya zao zinakuwa zimeimarika.
Pia ameeleza kuwa watambue kwamba wengi wao ambao hawajapata chanjo kabisa wanapitia msukosuko mkubwa wa afya na changamoto mbalimbali.
“Niwaombe chanjo zinaendelea kutolewa ndani ya Mkoa wa Mwanza,katika vituo vyetu vya kutolea huduma ya afya nendeni mkapate chanjo tunaendelea kumshukuru Mungu tunaona majira haya yanaunafuu kuliko majira yaliyopita kwa takwimu hali ya uchanjaji inazidi kuimarika siku hadi siku na kwa takwimu za masaa 24 yaliyopita tulichanja watu zaidi ya 30,000,”ameeleza Mhandisi Gabriel.
Kwa upande wake mmoja wa wananchi wa Mkoa wa Mwanza Suleiman Shagata,ameeleza kuwa wakati ugonjwa wa corona unaingia nchini kati ya makundi yaliyokuwa yapo hatarini ni pamoja na kundi la wazee na wenye magonjwa sugu.
Hivyo kwa kuzingatia hilo Serikali baada ya kuanza kutoa chanjo ya uviko-19 ilitoa kipaumbele kwa wazee ambapo na yeye ni miongoni mwa wazee waliopata chanjo hiyo mara tu zoezi hilo lilipoanza mkoani Mwanza.
“Zoezi la utoaji chanjo ya uviko-19,lilivyoanza mkoani Mwanza nilikuwa mstari wa mbele kupata chanjo hiyo kama mzee na baada ya kupata sijaona mabadiliko yoyote katika mwili kama vile watu walivyokuwa wanatuaminisha, changamoto ya corona bado ipo hivyo watu wapate chanjo hiyo,”ameeleza Shagata.
Ameeleza kuwa sababu ya kuwa mstari wa mbele kupata chanjo hiyo kwanza ni kutokana na Rais Samia kuanza kwa kupata chanjo pia zipo mamlaka nchini kama TMDA na TBS ambazo zinafanya uchunguzi wa dawa hizo kabla ya kuruhusu watu kutumia pia na wataalamu wa afya waliweza kutoa elimu na akaielewa hivyo kukubali kuchanjwa.
Hata hivyo Waziri wa Afya Ummy Mwalimu amebainisha kuwa Serikali kupitia Wizara ya Afya imelenga kufikia asilimia 70 ya watu waliochanja ikiwa ni sehemu ya mkakati wa Dunia wa kupambana dhidi ya ugonjwa wa UVIKO-19.
Ambapo Ummy akizungumza hayo Julai 6,2022 jijini Dodoma wakati akizungumza na wandishi wa habari mara baada ya kumalizika kwa kikao pamoja na Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa, ambaye ni kiongozi wa masuala ya chanjo dhidi ya ugonjwa wa Covid- 19. Ted Chaiban.
Ameekeza kuwa Tanzania ikiwa ni mwanachama wa shirika la Afya Duniani (WHO) na Umoja wa mataifa inaungana na mataifa yote ulimwenguni kuweza kupata kinga ya jamii dhidi ya Uviko-19 kwa angalau asilimia 70 ya watu wote duniani na hadi kufikia Julai 5,2022 Tanzania imefanikiwa kuchanja watu milioni 8.5
Naye Katibu Mkuu Msaidizi wa Umoja wa Mataifa na Mratibu
Mkuu wa Mpango wa utoaji chanjo ya Uviko-19 ,Ted Chaiban, ambaye yupo nchini Tanzania kwa ziara maalumu ya siku nne,amesisitiza kwamba janga la uviko-19, bado lipo na kwamba hatari ya kuibuka aina mpya ya virusi, hasa kwa makundi ambayo bado hayajapata chanjo ni kubwa.
“Janga la UVIKO-19 bado lipo kati yetu na hatuna budi kuwaambia tunawalinda wale walio hatarini zaidi, wakiwemo wazee, watu wenye maradhi sugu, watumishi wa afya walio mstari wa mbele na wale wanaofanya kazi katika sekta za utalii na hoteli,chanjo ndio kinga yetu madhubuti dhidi ya UVIKO-19 hakuna aliye salama hadi sote tuwe salama kama wanavyosema katika
Kiswahili.’Ni ujanja kuchanja,” ameeleza.
More Stories
AZAKI yawasilisha mapendekezo yao kwa Serikali katika kuboresha Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050
CP.Wakilyamba :Uvamizi maeneo ya hifadhi ya taifa katavi haukubaliki
Watu wawili wanaodhaniwa majambazi wapigwa risasi na Polisi