November 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Ofisa Mkuu wa Masoko na Huduma za Wateja kutoka NHIF, Luhende Singu akielezea vifurushi vya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya(NHIF) katika Maonesho 44 ya Biashara ya kimataifa 77 yanayofanyika katika Viwanja vya Julias Nyerere Jijini Dar es salaam (Picha na Mwandishi wetu)

Wananchi washauriwa kutembelea banda la NHIF

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online, Dar es Salaam

WANANCHI wameshauriwa kutembelea banda Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya(NHIF) katika Maonesho ya 44 ya Kimataifa ya Biashara katika Viwanja vya Julius Nyerere jijini Dae es salaam ili kupata elimu sambamba na kujiunga na huduma hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari katika maonesho hayo, Ofisa Mkuu wa Masoko na Huduma kwa Wateja wa NHIF,Luhende Singu amesema katika viwanja hivyo wamekuwa wakitoa elimu pamoja na kufanya usajili wa wanachama wapya.

“Wananchi na Watanzania wote kwa ujumla na wasii kutembelea banda letu ili waweze kujiunga katika vifurushi vya bima kwani bima ya afya ni kinga dhidi ya janga la maradhi.

“Bima ya afya sio unafuu wa matibabu au unafuu wa gharama za matibabu baada ya mtu kuanza kuugua bali bima ya afya ni kinga dhidi ya janga la maradhi,” amesema Singu.

Amesisitiza kuwa kila mwanachi anapaswa kuwa na bima kabla ya kuanza kuungua ili kuweza kuepuka gharama kubwa za matibabu bila ya bima.

“Mtu anapaswa kukata bima kabla hajaanza kuungua inatokea mara nyingi mtu anakwenda hospitali akishaona gharama zinakuwa kubwa ndipo anakwenda kutafuta bima hapo anakuwa atafuti bima bali anatafuta unafuu wa matibabu,” amesema Singu.

Amesema katika Maonesho ya Sabasaba wamekuwa wakifanya usajili wa wanachama wapya kupitia kifurushi cha vifurushi vya bima ya afya.

Singu amesema vufurushi hivyo vinatoa fursa kwa mtanzania kujiunga bila ya kulazimika kupitia katika kikundi au kwa mwajiri.

“Katika usajili huu wa vifurushi umetegwa katika makundi matatu ambapo kundi la kwanza ni kuanzia miaka 18 Hadi 35 ambayo ada yao ya chini ni shilingi 192000 kupitia kifurushi Cha najali afya huku ada ya juu ikiwa ni sh. 516,000 kupitia kifurushi Cha natimiza afya”amesema Singu.

Alisema kwa kundi la pili ni kuanzia umri wa miaka 36 hadi 59 ambayo ada ya chini ni shilingi 240,000 na ada ya juu ikiwa 612,000.

“Kundi la tatu kuanzia umri wa miaka 60 na kuendelea ambayo ada ya chini ni shilingi 360000 huku hada ya juu ikiwa 984000 ambapo kupitia vifushi hivi mtu anaweza kuanzia ngazi ya zahanati mpaka hospital ya rufaa ya mkoa bila kuitaji rufaa yoyote”amesema Singu.