November 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

wananchi wampa kongole Rais Samia

Raphael Okello, Timesmajira Online,Mwanza

BAADHI ya wananchi wa Jiji la Mwanza wamempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuiletea Mwanza maendeleo.

Maendeleo hayo ni pamoja na mradi mkubwa wa uvuvi unaogharimu takribani bilioni 11.5 na boti 55 mradi uliozinduliwa Januari 30,2024 na Rais mwenyewe.

Ujenzi wa shule za sekondari , miundombinu ua barabara na miradi mingine.

Wakizungumza baada ya ujio wa Rais jijini Mwanza, wananchi hao wameeleza kuwa kutokana na jijini la Mwanza kuendelea kupiga hatua miongoni mwa majiji nchini wamedai wako nyuma ya Rais.

Mzee Mligiti ambaye ni mkazi wa mtaa wa Mabatini jijini Mwanza anaeleza kuwa kwa kutambua maendeleo ya jiji la Mwanza , Rais Samia alimteua Mkurugenzi Mchapakazi Aroun Kagurumjuli kuwa Mkurugenzi wa jiji la Mwanza.

Mligiti ambaye amewahi kuwa mtumishi serikalini alionesha kusikitishwa na baadhi ya watu wanaoeneza propaganda mtandaoni kuwa mkurugenzi huyo hafai kuongoza Jiji la Mwanza na kwamba hatua hiyo ni kurudisha nyuma juhudi za Rais Samia kuwaletea wanamwanza maendeleo.

Hata hivyo amesema hakuna haja ya kupiga kelele bali kazi iendelee na kama kuna tatizo vyombo vya uchunguzi vya serikali vipo viachiwe vifanye kazi.

Alfonce Magabiri na Deus Mwanuzi wanasema kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi mwaka 2022 Jiji la Mwanza lina watu zaidi ya 437,000 ambao wanamtegemea Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na wawakilishi wake akiwemo Aroun Kagurumjuli.