Na Mwandishi wetu, Timesmajira
WANANCHI wa kijiji cha Ikuvilo kata ya Luhota wilaya ya Iringa vijijini wametakiwa kujitokeza kwa wingi kuhakiki taarifa zao ili waweze kupiga kura katika uchaguzi mkuu ujao.
Hayo yamesemwa leo na Mdau wa Maendeleo na Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM),Wakili Sosten Mbedule mara baada ya kuhakiki taarifa zake huku aliwasisitizawananchi wa kijiji hicho umuhimu wa kuhakiki taarifa zao.
Amesema ni vema kila mwananchi kuhakiki taarifa zake ili aweze kutumia haki zake za msingi kuchagua viongozi wanaowataka.
“Wananchi wa kijiji cha Ikuvilo wanatakiwa kutumia fursa hii, kwenda kwenye kituo cha kupiga kura na kuhakiki taarifa zake, kuepuka usumbufu hapo badae,” amesema na kuongeza
“Wale ambao kadi zao zimeharibika au kupotea ofisa uchaguzi atawasaidia taratibu za kufanya ili wapate kadi mpya,” amesema Wakili Mbedule
Uchaguzi Mkuu wa Tanzania unaotarajia kufanyika mwezi Oktoba 2025, wa kumchagua Rais, Wabunge na Madiwani.
More Stories
Bodaboda wamchangia Rais Samia Mil 1 ya fomu ya Urais
HAYA HAPA MATOKEO YOTE FORM II NA DARASA LA IV
Ufaulu waongezeka matokeo ya Darasa la Nne na Kidato cha Pili