Na Mwandishi wetu,Timesmajira Online,Temeke
Wananchi wa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke mkoani Dar-es-Salaam,wametakiwa kulinda amani na kujiepusha na watu wenye nia mbaya ya kutaka kuivuruga kuelekea uchaguzi mkuu mwaka huu.
Hayo yamebainishwa Februari 12,2025 na Mkuu wa Mkoa wa Dar-es-Salaam Albert Chalamila,akizungumza na wananchi wa Temeke, siku ya pili ya ziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa na Serikali katika Halmashauri hiyo ikiwemo mradi wa stendi ya Buza na ukarabati wa soko la Temeke.
![](https://timesmajira.co.tz/wp-content/uploads/2025/02/IMG-20250213-WA0009-1024x682.jpg)
Chalamila,amesema amani iliyopo ni muhimu kwa maslahi ya umma ikiwemo shughuli za uchumi wa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla.
“Katika kuelekea uchaguzi mkuu vyama vya siasa,vimekuwa vikipita kwa wananchi kutoa sera zao, vipo vitakavyotumia fursa hiyo kuhubiri siasa za uvunjifu wa amani ya nchi, wananchi jiepusheni na sisa za namna hiyo,”amesema.
Sanjari na hayo amesema,mradi wa stendi ya Buza umekamilika huku daladala bado hazijaanza kuitumia,hivyo amemuagiza Mkuu wa Wilaya ya Temeke na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Temeke kukaa pamoja na LATRA na Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani, ili kuhakikisha daladala zinaanza kutumia stendi hiyo haraka iwezekanavyo.
Katika hatua nyingine Chalamila amewahimiza wafanyabiashara katika soko la Tandika kutumia fursa ya kufanya biashara kwa saa 24 kujiongezea kipato pamoja na kuwasisitiza kuwa nanutamaduni wa kulipa kodi na kutoa risiti kwa wateja wao.Huku akimuagiza Mkurugenzi kuendelea kufunga taa katika soko hilo na baada ya zoezi hilo zitafungwa kamera zitakazo saidia kudhibiti wahalifu.
![](https://timesmajira.co.tz/wp-content/uploads/2025/02/IMG-20250213-WA0007-1024x682.jpg)
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Temeke Sixtus Mapunda, amesema kuwa wanaendelea kufanya maboresho ya miundombinu katika soko la Tandika ikiwemo ufungwaji wa taa ili kufanikisha ufanyaji wa biashara kwa saa 24.
Mapunda ametumia fursa hiyo kutoa maagizo kwa madereva wa daladala kuanza kufika katika stendi ya Buza kama walivyokubalina.
![](https://timesmajira.co.tz/wp-content/uploads/2025/02/IMG-20250213-WA0010-1024x682.jpg)
More Stories
Dkt.Batilda:Tumeanza mazungumzo waliotelekeza viwanda wanyang’anywe
TMA:Kuna ongezeko la joto kwa baadhi ya maeneo nchini
Madiwani Kilindi wapongeza RUWASA utekelezaji miradi ya maji