November 6, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Wananchi Same waanza kupewa elimu kuhusu Kilimo cha mirungi

Na David John,TimesmajiraOnline

MAMLAKA ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya nchini (DCEA), kwa kushirikiana na ofisi ya mkuu wa Wilaya ya Same imetoa elimu kwa wananchi wa kata ya Tae wilayani Same mkoani Kilimanjaro kuhusu madhara ya kujihusisha na kilimo, biashara na matumizi ya dawa za kulevya aina ya mirungi.

Ni siku chache baada ya operesheni tokomeza mirungi iliyofanyika katika kata hiyo na kufanikisha kuteketeza hekeri 535 za mashamba ya Mirungi na kukamatwa kwa watuhumiwa tisa.

Elimu hiyo metolewa Julai, 11,2023 katika kikao maalumu kilichowahusisha maafisa wa DCEA, viongozi wa wilaya ya Same, wataalamu ya masuala ya kilimo na biashara pamoja na wakazi wa kata hiyo.

Akizungumzia athari za matumizi ya mirungi Kamishna wa Kinga na Tiba DCEA, Dkt. Peter Mfisi ameeleza kuwa matumizi ya mirungi yanachochea uhalifu ikiwemo ugomvi na mauaji kwa sababu ya kuathiri uwezo wa kufikiri, jambo inalosababisha mtu kuchukua maamuzi yoyote pasipo kutafakari matokeo yake na kusema kuwa baadhi ya maeneo ambayo kilimo cha mirungi yamekithiri kuna changamoto kubwa wananchi wake kitabia.

“Watoto wenu wakianza kutafuna mirungi mtazalisha kizazi chenye migogoro na mafarakano yasiyo isha,watu mtashindwa kutatua hata changamoto ndogo ndogo zinazowataka mkae chini na kuzijadili badala yake mnachukua mapanga na mikuki na kuanza kushambuliana” amesema Dkt. Mfisi.

Afisa kimo wa halmashauri ya Same, Mohammed Muhina ameyataja baadhi ya mazao ya biashara yanayostawi katika maeneo hayo yayoweza kuwa mbadala wa kilimo cha Mirungi.

“Eneo la Same linakubali mazao mbalimbali kama tangawizi, zao la vannila ambalo tayari limeanza kulimwa katika baadhi ya maeneo, lakini kuna zao la kahawa na mazao mengine mengi kama migomba na kadhalika” amesema Muhina.

Naye Kamishna wa Huduma za Kitengo cha Sheria DCEA, Veronica Matikila amesema Sheria ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya,Na. 5 ya Mwaka 2015 inakataza kilimo, kuhfadhi na kukusanya mazao haramu ikiwemo mirungi na bangi na adhabu yake ni kifungo cha miaka thelathini (30) jela au Kifungo cha masha.

Hivyo,yoyote anayejishughulisha kwa namna yoyote na dawa za kulevya anatendakosa na akibanika atachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria.

Aidha, Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Aretas Lyimo ametoa rai kwa viongozi wa halmashaur kuanzia maafisa tarafa nawenyeviti wa vitongoji kuwajia kakuhakikisha wanadhibiti uhalifu wa kiimo na matumz ya mirungi, pamoja na kutoa elimu kuhusu athari ya matumizi yake katika maeneo wanayosimamia kulingana na sheria za nchi.

“Ni wajibu wa kila kiongozi katika halmashauri kuhakikisha anadhibiti matumizi ya mirungi, ikwa ni pamoja na kukomesha kilimo chake kwa kutoa elimu kwa wananchi kuhusu shughuli mbadala wanazoweza kuzfanya ikiwemo kilimo cha mazao mengine yenye tija.

“Pia kuwatumia wataalam wa
halmashauri kutoa ujuzi kwa wananchi utakaowasaida kwa namna moja au nyingine kufanya biashara halali zitazokuwa chanzo cha mapato kwa ajili ya kujikimu na maisha na kuachana na biashara ya mirungi.”amesisitiza Kamishna Jenarali Lymo.

Katika hatua nyingine, Mkuu wa Wilaya ya Same, Kasilda Mgeni ameagiza viongozi wa kata ya Tae kuhakikisha ndani ya mwezi mmoja visiki vyote ving’olewe na mashamba yote ambayo hayakufikiwa wakati wa operesheni yateketezwe, ambapo utekelezaji wake umeanza tangu Julai, 12.2023 ukiongozwa na afisa mtendani wa kata ya Likweni Isaack Stephano Mwansasu.
Vilevile, mkazi wa kata ya Tae, Elsante Semkondo amesema asilimia kubwa ya vijana katika kata hiyo wanatumia mirung kutokana na tabia ya kuiga.

Hivyo,ameishukuru Serikai kwa kuwapa elimu kuhusu mirungi na dawa za kulevya kwa ujumla kwa kuwa itaongeza hamasa kuchukua hatua ya kudhibiti
changamoto hiyo na kuachana kabisa na kilimo cha mirungi.

Opereshen hiyo ya kutekeza mirungi katika mkoa wa Kilimanjaro ni hatua ya Serikali katika kuhakikisha nadhibti na kutokomeza matumizi ya dawa ya kulevyana imekuja ikiwa wiki kadhaa tangu kufanyika maadhimisho ya Siku ya Kupiga Vita Dawa za Kuevya mkoani Arusha ambapo mgeni rasmi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan aliagiza kufanyika kwa operesheni endeevu ikiwa ni pamoja na viongozi wote wa Serikali kushiriki katika kupambana na dawa za kulevya katika maeneo yao.

Katika kutekeleza maagizo ya Rais,Dkt.Samia, Mkuu wa wilaya ya Arumeru Emmanuela Kaganda akishirikiana na Mamlaka ya kudhibiti na kupambana na dawa za kulevya jana.

Amevipongoza Vyombo vya Ulinzi na usalama wilayani humo katika operesheni maalum katika kjiji cha Kisimiri na kufanikiwa kuteketeza gunia 280 na mbegu kilogramu 300 za bangi na kukamatwa kwa watuhumiwa nne wakihusishwana bangi hizo.