December 28, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Wananchi Mbulu watumia siku ya Kumbukizi ya DED Myenzi kwa kumpongeza utendaji wake wa kazi

Na Mary Margwe, TimesMajira Online, Mbulu

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mji wa Mbulu Mkoani Manyara Yefred Myenzi ( Mashine ya Kazi ) leo ametimiza miaka 50 ya kuzaliwa kwake ( Happy birthday to Him ).

Kufuatia kumbukizi hiyo, wananchi wa Mji wa Mbulu, watumishi pamoja na Mkoa kiujumla wamemtakia Mkurugenzi Myenzi maisha marefu yenye upendo, furaha na Amani, ili aweze kuendelea kuwatumikia kikamilifu wananchi wa Mji wa Mbulu.

Baadhi ya wananchi walisema Halmashauri ya Mji wa Mbulu ni Moja ya Halmashauri inayoendelea kufanya vizuri kwenye ukusanyaji mapato ya ndani kwa mwaka 2022Mkurugenzi wa Mji wa Mbulu, Yefred Myenzi ( Mashine ya Kazi ) hapo akipokea cheti cha kuongoza kitaifa kama Halmashauri iliyokidhi vigezo vyote saba vya upimaji ,tukio lililofanyika Mwaka Jana.

Hata hivyo mmoja wa wananchi hao Juma Hitler alisema Mkurugenzi huyo amekua ni chachu kubwa ya maendeleo katika Halmashauri hiyo Toka alivyohamia Mbulu akitokea Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro, hivyo wanampongeza Kwa kumbukizi ya siku yake ya kuzaliwa Kwa kumtakia maisha marefu huku wakimuombea ili aweze kuendelea kuwatumikia vema wananchi hao na hatimaye kuweza kutumiza malengo aliyokusudia Kwa wananchi wa Mbulu Mjini.