Na David John,Timesmajiraonline,Kilimanjaro
WANANCHI waishio katika vijiji vya Rikweni, Heikondi, Tae na Mahande vilivyopo Kata ya Same Mkoani Kilimanjaro wamesema wapo tayari kuachana na kilimo cha zao haramu la mirungi ili kuunga mkono juhudi za Serikali za kutokomeza madawa ya kulevya hapa nchini.
Pia wameiomba Serikali kuwapelekea wataalamu wa kuwapa mafunzo juu ya kilimo cha mazao mengine mbadala ili kuendelea kujipatia kipato Kwa njia halali na zinazokubalika na jamii.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti na waandishi wa habari mkoani humo hivi karibuni wamesema ardhi yao ina rutuba na kwamba wapo tayari kuachana kabisa na zao hilo haramu na kujikita kwenye mazao rafiki.
Ndani ya vijiji hivyo, Serikali kupitia Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA)kwa kushirikiana na Vyombo vingine vya Dola imeanza Oparesheni maalum ‘Tokomeza Mirungi’.
“Eneo letu asilimia kubwa ni wakulima wa kilimo hicho na wamekifanya huu mti kama wa biashara unaowaingizia kipato,” amesema Mkazi wa Kijiji cha Rikweni, Mchungaji Elisante Senkondo.
Nakuongeza kuwa “Mungu anakitumia kama chombo kinachomkemea anayefanya uasi wa aina yoyote, siyo tu mirungi, kama mauaji nakadhalilka.
“Niiombe Serikali itupe nafasi tukae na watu wetu katika makanisa tuwashauri kwa nguvu zaidi ili kwa hiyari yao wenyewe waweze kukubali kutokomeza hizi dawa za kulevya.”Amesema Senkondo
Kwaupande wake Mwalimu Janeth Sarambo wa Shule ya Msingi Rikweni amesema wananchi wameathirika mno kwa kilimo hicho kijijini humo hivyo Kuna haja ya Serikali kuendelea kuchukua hatua ili kuimarisha afya za watanzania.
Ameongeza kuwa Mwanzo walikuwa hawajagundua ni dawa za kulevya sasa wamegundua,, hivyo wanaiomba Serikali ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan iwaletee wataalamu wa kilimo ili wananchi wapewe elimu kuhusu kilimo cha mazao {mengine}.
“Tunaotesha migomba, mahindi, maharagwe ni mazao machache tu hayakubali huku, tunaomba Serikali itusaidie ili wananchi wasipate mahangaiko, walime mazao mazuri wapate biashara na fedha ili wasihangaike na mirungi.”Amesema
Naye Kaimu Afisa Mtendaji wa Kata ya Tae, Japhet Msengi ameongeza “Tumekuwa tukipambana kwa ajili ya kusaidia jamii inayotuzunguka juu ya athari ya kilimo hiki, kimekuwa cha muda mrefu kwenye kata hii.
“Tulishapokea barua kwa Mkuu wa Wilaya na Mkurugenzi kwamba tuungane na viongozi wengine kutokomeza kwa njia ya kuwapa elimu ili ufahamu wa wananchi ubadilike.
Nakufafanua kuwa “Tulifanya hivyo kwa muda usiopungua miaka sita tangu tuanze hizi oparesheni, baadhi walipunguza na wengine waliendelea kwa madai kwamba kinawanufaisha na kupata pesa.wanadai si kwa ajili ya matumizi bali kuwapatia kipato, tulijaribu ku-organize na taasisi nyingine za kilimo ili kuwasaidia zao mbadala waondokane nacho.
Amesema ni kilimo ambacho hakiipatii mapato kata hiyo wala Serikali kwani si biashara halali huwezi kumkatia mti wa mirungi kwa sababu si biashara halali, wakati mwingine wanahangaika kupata mapato kwa kukata risiti na Serikali iweze kupata kodi.
Naye, Diwani wa Kata ya Tae Samwel Mbwambo amesema Serikali ina nia njema na wananchi wa Kata hiyo, lengo lake ni kusababisha wananchi waachane na kilimo hicho kinachosababisha wapate madhara makubwa lakini pia jamii kupoteza mwelekeo, ilani ya CCM 2025 ilishaandika utokomezaji wa dawa za kulevya ni sehemu ya wajibu wa Serikali.
Amewasihi wananchi wa Kata hiyo wasiendelee na kilimo hicho kitawaletea madhara makubwa mtafungwa kifungo ambacho ni kikubwa na jamii itapoteza nguvu kazi, vijana wakienda kwenye kifungo itakuwa imeisha.
“Niwaombe tuendelee na vilimo vingine ambavyo vitaweza kutusaidia katika uchumi wa familia zenu na kuacha na hili ambalo ni tatizo kubwa katika jamii hii.
Ametoa rai kwa wananchi hao pia kuhudhuria mikutano ya uelimishaji itakayofanyika ili wapate uelewa utakaowasaidia kubadilika, wananchi hao wametegemea kilimo hicho kwa sababu hawajapata elimu ya kilimo kingine, watusaidia ili tupate mabadiliko makubwa na kizazi kitakachokuwa kizuri.
“Itusaidie kutoka kilimo cha mirungi na kwenda kwenye kilimo kingine, kabichi, nyanya, vitunguu vinakubali vizuri.Mazao ya kimkakati kama parachichi inayouzwa bei kubwa nchi za nje, kwanini tusihamie kwenye kilimo hicho.nawasihi tubadilike twende kwenye kilimo kizuri ambacho hakisababishi watu kukimbia nyumba, kukimbia opareshe, tuachane na hili ili tuwe wananchi wema,” amesisitiza Samweli
More Stories
Waziri Jerry afanya uteuzi wa Makamu Mwenyekiti, Wajumbe watano wa bodi ya Shirika la Posta
Kapinga atoa maagizo TANESCO ,kuhusu Vijiji vinavyolipia gharama ya mijini kuunganisha umeme
Ukiukaji wa Uhuru wa Kidini na Kutovumiliana Huzusha Malumbano ya Kimataifa