Agnes Alcardo,Timesmajira Online,Dodoma
IKIWA leo ni siku ya mwisho ya kujadiliwa kwa bajeti ya Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), baadhi ya wananchi mkoani Dodoma wamejitokeza kutoa maoni yao kuhusu bajeti hiyo kwa mwaka wa fedha 2025/2026 yenye kiasi cha shilingi tirioni 11.7.
Akizungumzia bajaeti hiyo mkazi wa Dodoma, Maria Julius ambaye ni fundi cherehani amesema kuwa, anatamani bajeti ya TAMISEMI ilenge zaidi kwenye TEHAMA, ambapo itawarahisishia wafanyabiashara kujitangaza kupitia mitandao ya kijamii kwani kwa sasa Dunia ipo kiganjani.

“Mfano mimi nikishona nguo zangu huwa naweka kwenye mitandao ya kijamii ili niweze kuwafikia watu wengi zaidi na kuona kazi zangu, kwahiyo natumai TAMISEMI itatusaidia kwa upande huo,”amesema Maria.
Emmanuel Mabalwe amesema kuwa, amefuatilia Bunge na kuona bajeti ya mwaka wa fedha 2025/2026, iliyowasilishwa na Waziri wa TAMISEMI, Mohammed Mchengerwa, imekuwa na ongezeko kwa kiasi kikubwa kutoka bajeti ya mwaka jana 2024/2025 ambayo ilikuwa tirioni 10.1 hadi tirioni 11.7
“Tirioni 1.66 ndiyo ambayo imeongezeka kwa mwaka huu na hiki ni kiwango kikubwa ambacho kitaenda kuhudumia watanzania wote kwa ujumla, kwa hali hiyo tunaipongeza sana Serikali yetu” amesema.
Aidha kwa upande wake Manoa Samweli, amesema bajeti ya TAMISEMI ijikite kwenye masuala ya michezo kwani mpaka sasa imekuwa ajira kwa vijana wengi ambao wana vipaji.

Pia amesema kuwa, mchezo wa mpira wa miguu unazidi kukua hivyo inatakiwa kuwepo na maboresho zaidi hasa kwenye miundombinu ya michezo kama vile viwanja, jambo litakalosaidia kutoa ajira kwa vijana ambao wana vipaji vya mpira
More Stories
Kapinga :Vitongoji 82 Tarime vijijini kupelekewa umeme na mradi wa HEP IIB
Watanzania wana wajibu kuhakikisha urithi wa utamaduni wa Taifa unalindwa
Mbunge Buhigwe aomba wataalam wa mionzi