November 16, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Wananchi Dodoma waahidi ulinzi mradi wa Vanilla

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

Mkurugenzi Mkuu wa makampuni ya Vanilla Internation Limited na mvumbuzi wa miradi mikubwa ya kilimo cha vanilla Zanzibar na Dodoma, Arusha, Mwanza na nchini Dubai na Vanilla Comoro na BWANA Simon Mnkondya, amewata wananchi kuendelea kuwekeza katika miradi yake ya vanilla kwani inautajiri mkubwa.

Ameyasema hayo Jana Jijini Dodoma wakati wa mashindano mbalimbali ya kimichezo na sanaa, burudani kwa ya kujenga mahusiano madhubuti kati ya kampuni na Mradi wa Vanilla Village ya Mkoa huo na Wananchi hususani wanakijiji cha ZAMAHERO MAYAMAYA.

Kwa upande wa Mwekezaji huyo bwana Simon Mnkondya, amewahasa vijana na wananchi kwa ujumla kuchangamkia fursa ya uwekezaji wa vanilla kwani za kilimo mkombozi wa uchumi Tanzania na hususani kwa Dodoma na pia amesema ameitisha burudani hiyo kwa sababu vanilla inahitaji ulinzi na bila mahusiano mazuri na Wananchi mradi wa vanilla.

Ameeleza kuwa, vanilla ni zao linaloongoza kwa kuibwa duniani kutokana na ukubwa wa bei ya vanilla inayofikia mpaka milioni moja licha ya kipindi kifupi cha kushuka kwa bei kutokana na ugonjwa wa Korona.

Amewataka wananchi wawe na namba zake ili kupata mafunzo namba hizo ni 0769300200 au 0629300200 au 0624300200.

Kwa upande wa Mwenyekiti wa kijiji wa Zumahero Wilson amekiri kuridhishwa na uhusiano uliopo kati ya mwekezaji huyo na wanakijiji wake.

Naye Lupakisyo Yeremia amesema ni mwekezaji wa kuigwa kwa ushirikiano na wananchi hapa dodoma.

Zaidi ya mia mbili wameshiriki michezo mbali mbali ikiwemo: unywaji wa soda bila kuvuta futo/ kuguda, kucheza michezo ya kurusha chupa, mpira wa miguu danadana , unywaji wa wines za vanilla na uimbaji wa mziki na kupata fursa ya maswali ya matumizi ya vanilla.

Wananchi wa Dodoma wameufurahia sana mradi wa vanilla dodoma na kuahidi kutoa ushirikiano wa kiulinzi na ufanyaji wa kazi kwa maana mradi umeonekana kuwa chachu ya ajira kwa kanda ya Kati Dodoma hususani kwa vijana wa vijiji vinavyouzunguka mradi wa vanilla village dodoma.