Na Queen Lema, Arusha
Wananchi zaidi ya 200 kutoka maeneo mbalimbali hapa nchini wamefanikiwa kupewa elimu sahihi ya matumizi ya ardhi pamoja na namna ya kumiliki ardhi
Aidha mbali na kupewa elimu hiyo lakini pia wananchi hao wameweza kupewa mbinu mbadala za kunufaika na ardhi zao
Elimu hiyo imetolewa Kwa wananchi hao ili waweze kuwa wamiliki wa ardhi lakini pia kufanya matumizi sahihi ya ardhi kwa wakati husika
Hayo yameelezwa Estomih Samanga ambaye ni Mkurugenzi wa kampuni hiyo ya Estomih Samanga Real Estate iliopo Intel Jijini Arusha wakati akizumgumza na waandishi wa habari ofisini kwake Juzi juu ya umuhimu wa kumiliki ardhi
Amesema kuwa wananchi hao Ambao walipewa elimu hiyo waliweza kutambua Mambo mbalimbali ambapo Hapo awali walikuwa hawajui
“Unajua kuna mtu ambaye yupo tu hajui kuwa ardhi ni hazina ambayo inalipa na kupanda gharama siku baada ya siku,lakini ardhi ni mtaji unapokuwa na ardhi yako unaweza hata kuaminika na taasisi nyingine za kifedha”ameongeza
Wakati huo huo amesema kuwa katika elimu ambayo wameitoa pia imeweza kuwasaidia wananchi kutambua hata Aina ya udongo mzuri wa kujengea kwani Kwa sasa wapo baadhi ya wajenzi ambao wanajenga nyumba za Kudumu au za biashara lakini baada ya muda mfupi zinabomoka hili pia tumewafundisha,”ameongeza
Katika hatua nyingine amesema kuwa Kwa sasa wamejipanga kuhakikisha kuwa wanaendelea kutoa huduma ya umiliki wa ardhi,Kwa Njia ambayo ni raisi Sana ili kila mtanzania aweze kujipatia ardhi
“Ndani ya jamii kuna makundi mbalimbali lakini tumeweka malengo ya kuhakikisha tunayafikia makundi hayo Kwa Njia Raisi Sana ambapo Kwa hivi Karibuni tutafanya semina kwa makundi ya wajasirimali wa masokoni”ameongeza
Amehitimisha kwa kusema kuwa vijana nao kwa sasa wanatakiwa kutumia fursa hiyo kuweza kumiliki ardhi kwa njia ya malipo ya kidogo kidogo ili kuraisisha maisha ndani ya familia zao.
More Stories
AAFP yampitisha Ngombare Mwiru kugombea Urais Bara
DC Mpogolo:DMDP kujenga barabara za urefu km 67 Ilala
Uhakiki na uchambuzi wa kazi za waandishi wa tuzo za Samia Award wafanyika kwa weledi