December 26, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mgombea ubunge Jimbo la Ludewa Joseph Kamonga aliyevaa miwani akijumuika na wananchi wa Kijiji Cha Ngalawale kata ya Ludewa kupata kinywani cha kabila la wapangwa baada ya wananchi kuzuia barabara wakati akitoka katika Kijiji Cha Nkomang'ombe kwenye mkutano wa kampeni .Picha na David John

Wanakijiji Nkomang’ombe waombwa kumchagua Dkt.Magufuli

Na David John,TimesMajira,Online Ludewa

MGOMBEA Ubunge ambaye amepita bila kupingwa katika Jimbo la Ludewa,Joseph Kamonga amefanya mkutano mkubwa katika Kijiji Cha Nkomang’ombe wilayani humo huku akiwataka wananchi wa jimbo hilo kumchagua Mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi CCM Dkt John Magufuli kwani ndio mtu sahihi.

Amesema kuwa yeye ni mtoto wao na anawapongeza wananchi hao kwakumwezesha kupita bila kupingwa lakini kazi kubwa iliyopo mbele nikuhakikisha wanampa kura za kutosha Rais Dkt Magufuli.

Kamonga ameyasema hayo Kijijini hapo leo akiongea na wananchi wa jimbo hilo ambapo kwa asilimia kubwa wananchi hao wameonyesha imani kubwa na CCM ,Rais Dkt John Magufuli na kwake kama mbunge kupitishwa kwenye kura za maoni .

“Ndugu zangu nipo mbele yenu kwa ajili ya kumuombea kura ,Rais Dkt. magufuli kwani amefanya mambo makubwa sana ikiwa pamoja kuleta meli ziwa nyasa pamoja na kutengeneza barabara za kiwango cha lami kutoka Ludewa hadi Njombe.

Amesema kuwa mbali na barabara hiyo,pia kuna barabara zingine ndani ya wilaya hiyo pamoja na mkoa wa Njombe zitawekwa lami hivyo Chama hicho kimejipanga kuwajali wana Ludewa.

Kamonga amesema Rais Dkt Magufuli ameweza kuwasomesha watoto elimu pasipokuwa na malipo na kujenga madarasa 36.

Pia Rais Dkt Magufuli amejenga nyumba za walimu,mabweni huku kwenye sekta ya maji ametumia bilioni 4 kwa ajili ya ya maji ndani ya wilaya ya Ludewa hivyo amewataka wananchi hao kuelewa kwamba Mkuu huyo wa nchi anawapenda Sana.

“Nataka niwaeleze kuwa Rais Magufuli ni jembe na Ludewa anatupenda sana angalia miradi hii yote ambayo ametuletea ni wazi kwamba anatujali na kutupenda sana hivyo nawaomba tumchague diwani Eliya Maganga pamoja na Dkt Magufuli kuwa Rais wa nchi kwa Mara nyingine “amesema Kamonga

Aliwataka wananchi hao kuwa na imani na mgombea huyo udiwani wa kata ya Nkomang’ombe kwani changamoto za kata hiyo anazijua sana na yeye yupo tayari kushirikiana naye akiwa kama Mbunge wa Jimbo hilo ambaye amepita bila kupingwa.

Mgombea ubunge alitumia mkutano huo kuahidi kushughulikia baadhi ya changamoto ambazo zipo kwenye baadhi ya maeneo ikiwamo vijiji na masuala fidia kwenye maeneo ambayo yamepitiwa na miradi ya serikali .

Naye mgombea udiwani wa Kata Nkomang’ombe,Maganga amewaomba wananchi wa Kijiji Cha Nkomang’ombe kuhakikisha oktoba 28 wanampa kura Dkt Magufuli katika nafasi ya urais na yeye kama diwani wao.