George Mwigulu,Timesmajiraonline,Katavi.
WAZIRI Mkuu Mstaafu na Mwenyekiti wa kamati ya ushauri kwa Rais katika masuala ya kilimo na chakula,Mizengo Pinda amewaonya viongozi na makampuni yaliyopewa dhamana ya kusimamia na kusambaza mbolea za rukuzu kwa wakulima kuacha matumizi mabaya ya madaraka yanayo zorotesha matumizi ya mbolea kwa kasi ili kukuza uzalishaji wa mazao mbalimbali.
Matumizi mabaya madaraka kwenye usambazaji wa mbolea kwa wakulima ni hali ya wasimamizi walipewa dhamana na serikali kuwadanganya wakulima kuwa mbolea hazipo kwa lengo ya kuzipeleka mahala pengine kwa ajili ya watu fulani na kusababisha kero kwa wakulima hao kushinda asubuhi hadi jioni wakitafuta mbolea.
Akizungumza leo na wadau wa kilimo katika ukumbi wa Mpanda Social Hall Manispaa ya Mpanda Mkoa wa Katavi ikiwa ni sehemu ya maazimisho ya wiki ya Mwanakatavi alisema kuwa ili kufikia asilimia 10 ya sekta ya kilimo kuchangia pato la taifa ifikapo mwaka 2030 suala la matumizi ya mbolea,mbengu bora na uhifadhi bora wa mazao unatakiwa kuzingaitiwa.
Pinda amesema kuwa hivi sasa kwenye sekta ya kilimo matumizi ya mbolea yako chini na hii inachangiwa na baadhi ya wasimamizi waliopewa dhamana na serikali ya kusimamia utoaji wa mbolea kwa wakulima kutumia madaraka yao vibaya kuhujumu usambazaji wa mbolea kwa wakulima.
Serikali imekubali kubeba mzingo wa kutoa ruzuku kwa ajili ya mbolea na kinachohitajika ni usimamizi wa upatikanaji wa mbolea hizo ” uzoefu wa mara ya mwisho hali haikuwa nzuri kwa baadhi ya maeneo,sehemu zingine unakwenda huko unakuta viswahili mbolea zipo lakini watu wanazungushwa kuanzia asubuhi hadi jioni ooh mbolea haijafika kumbe muongo yeye ameshatengeneza line nyingine mbolea hiyo anataka iende kwa fulani”.
Akiwa mwenyekiti wa kamati ya kumshauri rais kwenye kilimo na chakula.Pinda amesema kazi waliyonayo ni kupitapita katika maeneo ya nchi kubaini chanzo hasa cha vikwazo vinavyofanya kushindwa kufikia lengo la kuwa ghara katika bara la Afrika kwenye uzalishaji wa mazao ya chakula ” kuja kwangu hapa nami nimefaidi kuona baadhi ya vikwazo hivyo”.
Amesema kuwa matumizi ya mpegu bora ni wakati sasa umefika kwa taasisi zinazosimamia ubora huo kuongeza usimamizi zaidi ili kudhibiti na kutokomeza tabia hiyo ambayo ni chanzo cha uzalishaji mbaya wa mazao ” kuna watu wanatabia ya kuchugua mpegu za kawaida na kuzipaka rangi na kuzifunga kwenye mifuko vizuri kumbe ni fake”
Katika ubora zana za matumizi ya kilimo kuna umuhimu wa jamii kupewa elimu zaidi kuachana na kilimo cha jembe la mkono na kukeukia kilimo cha matrekta ambacho kina tija kubwa kwenye uzalishaji.
Aidha amebainisha kuwa bado kuna changamoto kwa maafisa ugani kushindwa kupanga matumizi bora ya ardhi hususani kwenye ngazi za chini jambo ambalo linachochea zaidi migogoro ya ardhi ambapo maafisa hao wametakiwa kusimamia matumizi bora ya ardhi pamoja na kutatua migogoro kati ya wakulima na wakulima.
Mkuu wa Mkoa wa Katavi,Mwanamvua Mrindoko amesema kuwa mkoa wa Katavi katika msimu ujao wa kilimo 2023/2024 umejipanga kulima Hekta laki tatu na sitini na sita elfu za mazao mbalimbali ili kuongeza uzalishaji wa mazao hayo na kukuza uchumi wa mkoa kupitia sekta ya kilimo.
Kuhusu matumizi ya dhana za kisasa za kilimo hususani Matrekta kwa wakulima wa mkoa wa Katavi ameeleza kuwa hadi sasa kuna kiwango kidogo sana cha wakulima kutumia kutumia vifaa vya kisasa katika kilimo cha mazao hayo kwa mkoa wa katavi.
Raymond Kamtoni Mkulima wa mkoa wa Katavi amesema kuwa ili kufikia asilimia 10 ya sekta ya kilimo kuchangia pato la taifa ifikapo mwaka 2030 serikali inapaswa kudhibiti mbolea zisizo na ubora pamoja na viuatilifu.
Mkulima huyo amesema mbolea na viatilifu visivyo na ubora ni chanzo kikubwa sana cha kinachokwamisha juhudi za mkulima kujikwamua kiuchumi na kama kitadhibitiwa lengo la serikali kwenye sekta ya kilimo kutoa mchango kwenye pato la taifa utafanikiwa.
More Stories
CCM imejipanga kushinda kwa kishindo
Wanaotumia lugha za matusi,kashfa kwenye kampeni waonywa Â
Polisi Mbeya yawataka waandishi wa habari kutoa taarifa sahihi