Na David John, timesmajira,online
MWANAHABARI ambaye pia ni Mhariri wa Magazeti ya Kampuni ya New- Habari 2006
,Bakari Kimwanga leo amechukuwa fomu ya kugombea Udiwani kata ya Makurumla Manispaa ya Kinondoni.
Akizungumza Mara baada ya kuchukuwa fomu amesema kuwa anakipongeza na kukishukuru Chama chake kuweka mfumo wa wazi wa uchukuaji fomu.
Katibu wa Kata hiyo, Sarama Mlaponi amesema mchakato wa uchukuaji wa fomundani ya Kata hiyo mpaka leo huu takribani wanachama zaidi ya kumi wamejitokeza kuchukua fomu za udiwani.
Amesema mwamko upo japo sio mkubwa kwani hadi Jana walikuwa watatu lakini kufika leo idadi inaongezeka na sasa wamefikia zaidi ya kumi na kwamba upande wa wanawake ni mwanamke mmoja ambaye amejitokeza.
Wakati huohuo Mwandishi Mkongwe kutoka vyombo vinavyomilikiwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM), Angella Akilimali amechukuwa fomu ya kuomba ridhaa ya kuwania ubunge wa Jimbo la Ukonga Jijini Dar es Salaam .
Angella amechukuwa fomu hiyo leo julai 15 katika Ofisi za CCM wilaya ya ilala Jijini hapa ambapo amesema amejipima ,amejitafakari nakuona anafaa kuchukua fomu.
Hata hivyo amefafanua kuwa kwamujibu wa Chama Chao kimetoa ratiba ya uchukuaji na urejeshaji fomu ,hivyo huu si wakati wa kuzungumza chochote bali wakati utakapofika nakupata ridhaa kutoka kwenye Chama chake atakuwa na chakueleza.
“Chama kimetoa ratiba ya uchukuaji na urejeshaji fomu kwamba mwisho julai 17 mwaka hivyo anakwenda kuijaza na Kisha kuirejesha kwa wakati ili kuacha Kura ya maoni itaamua na nani atapeperusha bendera ya Chama .”amesema angella
More Stories
Mpango ashiriki mazishi ya Mama yake Serukamba
TRA kuongeza idadi ya waendesha uchumi walioidhinishwa
TRA Tanga wajivunia ukusanyaji mapato