September 18, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Wanafunzi shule ya msingi wapewa chakula

Na Herishaban, TimesMajira Online

Serikali ya Mtaa Kalume imetoa chakula bure cha wanafunzi zaidi ya 300 wa darasa la saba leo na kesho wanaofanya mtihani wa kuitimu elimu ya msingi shule ya msingi Ilala Boma na Mkoani .

Akizungumza wakati wa kugawa chakula kwa wanafunzi wa shule ya Ilala Boma Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa Kalume Hajji Bechina, alisema utaratibu wa kurisha chakula bure kwa wanafunzi kwa shule ya Ilala Boma na Mkoani ni endelevu kila mwaka .

“Serikali ya mtaa Kalume Ilala kwa kushirikiana na chama cha Mapinduzi CCM tawi la Shauri moyo tumeweka utaratibu wetu wa kulisha chakula bure shule za kata ya Ilala ,Ilala Boma na Mkoani kugawa chakula bure kila mwaka katika kuunga mkono juhudi za Serikali ya awamu ya sita ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan “alisema Bechina

Mwenyekiti Bechina alisema Serikal ya Mtaa Kalume imewapunguzia Wazazi mzigo watoto wao siku mbili za mitihani wanakula chakula bure kinachogharamia na Ofisi ya Serikali ya Mtaa kuanzia chai asubuhi na chakula cha mchana kila mwaka.

Alisema pia wasimamizi wa shule hizo mbili wanaosimamia mitihani pia wanakula chakula bure kinachoandaliwa na Serikali ya Mtaa Kalume.

MWENYEKITI BECHINA aliwatakia khery darasa la saba wafanye vizuri mitihani yao kwa siku hizo mbili.

Alisema Serikali ya Mtaa Kalume inaunga mkono sera ya Serikali ya elimu bure na kuwawezesha wanafunzi chakula na kuweka mazingira bora ya shule za Ilala Boma na Mkoni Wilayani Ilala.