September 30, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Wanafunzi waliokosa sifa za kujiunga na kidato cha kwanza wapatiwa fursa vyuo binafsi

Na Esther Macha, Timesmajira, online,Mbeya

SERIKALI mkoani Mbeya imesema wanafunzi waliokosa sifa za
kujiunga na kidato cha kwanza katika shule za serikali wamepatiwa fursa ya kujiunga na vyuo vya ufundi stadi (Veta) katika vituo mbali mbali hususan vinavyomilikiwa na watu binafsi.

Homera amesema kuwa katika kundi hilo pia wapo wanafunzi ambao watajiunga na elimu ya mfumo wa Memkwa kwa lengo la kuondokana na taifa kuwa na makundi ya watoto wa mitaani ,ajira
katika umri mdogo .

Mkuu wa mkoa wa Mbeya ,Juma Homera amesema hayo leo wakati akitoa
taarifa ya masuala ya elimu kwa wanafunzi ambao hawajachaguliwa
kidato cha kwanza 5,236 na mikakati ya mkoa ilivyojipanga kwa
wanafunzi waliokosa nafasi.

Homera amesema kuwa katika mkoa wa mbeya 5,236 walipata madaraja B
na E hawakuwa na sifa za kujiunga na elimu ya kidato cha kwanza katika
shule za serikali walikaa na watalaam waliamua kuwapanga kwenye vyuo
mbali mbali vya ufundi na elimu ya watu wazima .

Amesema sababu ya kuwapanga kwenye vyuo hivyo ni kutekeleza Ilani ya
chama chama cha mapinduzi ya mwaka 2020 /2025 iliyolenga kuboresha
ubora wa elimu
hususani elimu ya ufundi ,mafunzo ya ufundi stadi hii ikiwa ni
pamoja na utoaji elimu nje ya mfumo rasmi (MEMKWA)ili kuwawezesha
walikosa sifa za mfumo rasmi kuweza kutimiza ndoto zao za kielimu .

Aidha Homera amesema kuwa kitu kingine kilichopelekea mkoa kufanya
hivyo ni pamoja na kupunguza vijana wasio na kazi mitaani ambapo
hugeuka kuwa wahalifu katika jamii mfano panya riad , nyuki .

Amesema ni vema watoto wote 3,236 waliokosa fursa za kujiunga na
kidato cha kwanza wajiunge kwenye vyuo vilivyopo ndani ya mkoa wa
Mbeya sababu nyingine ni kuongezeka kwa mzunguko wa fedha kwenye
jamii ambapo wataongezeka mafundi umeme , wapishi ,na mafundi wengine
muhimu watapatiwa elimu hiyo.

Amesema katika vyuo vilivyopo mkoani mbeya kila chuo
kimepewa idadi ya wananchi ambapo kwa wilaya Kyela kuna vyuo 19
watachukuliwa wanafunzi 746,Busokelo wanafunzi 421, Chunya wanafunzi
80, Mbarali vyuo 7 .

Kwa Upande wa Mbeya Jiji wanafunzi 1,205,
661 na Mbeya vijijini wanafunzi 1,634 na Rungwe wanafunzi 489 ambapo
jumla ya vyuo vyote ni 52 hivyo kufanya idadi ya wanafunzi wote 5,236
waliokosa nafasi kupata nafasi za kujiunga na elimu ya ufundi

Kwa upande wake Ofisa elimu Mkoa wa Mbeya, Ernest Hinju amesema kuwa
kwa mkoa wa mbeya walioripoti shule ni asilimia 86 hivyo kuna asilimia
14 tu ambao hawajaweza kuripoti shule wadau wa elimu wahimize watoto
waliobaki waripoti shule.

Aidha Hinju amesema kuhusu matokeao ya kidato cha nne wameendelea
kufanya vizuri kwa kuongeza ufaulu kutoka asilimia 89 mpaka 90.