Na Joyce Kasiki,Timesmajira online,Dodoma
KUFUATIA kuibuka kwa uwepo wa mafundisho na vitabu vyenye mafundisho kinyume na maadili ya kitanzania,Serikali kupitia Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia imefungua kituo cha huduma kwa wateja kwa ajili ya kutoa taarifa zinazokiuka miongozo na maadili katika taasisi za elimu.
Aidha amewasisitiza wamiliki wa shule kuhakikisha wanafuata Waraka Namba nne ambao unatoa muongozo katika shule zote nchini kuzingatia ubora wa elimu inayotolewa vinginevyo hatua kali zitachukuliwa kwa wahusika ikiwemo kufungia usajili wa shule husika.
Akizungumza leo Februari 3,2023 na waandishi wa habari Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt.Francis Michael amewaomba wananchi watoe taarifa kupitia simu ya mezani ya wizara hiyo yenye namba 0262160270 pamoja na simu ya mkononi namba 0737962965 .
āKupitia kituo hiki tunawasihi wananchi watupe taarifa mbalimbali za ukiukwaji wa maadili katika taasisi zote za elimu kuanzia shule za msingi hadi vyuo lakini pia watupe taarifa zote zinazohusiana na masuala ya ukatili katika maeneo ya shule zetu ili tuweze kuchukua hatua stahiki kwa wahusika kwa lengo la kumlinda na kumkinga mtotoāamesema Dkt.Michael
Aidha kuhusu vitabu vyenye mafundisho yaliyo kinyume na maadili Dkt.Francis alisema,Wizara ilitoa waraka namba 4 ambao unatoa muongozo katika shule zote nchini kuzingatia ubora wa elimu inayotolewa.
āWizara katika kutekeleza wajibu wake kwa kusimamia utoaji wa elimu nchini na katika kuhakikisha kuwa njia mbalimbali za ufundishaji na ujifunzaji zinazingatia ubora,maslahi ya nchi,mila ,desturi na tamaduni za watanzania ilitoa waraka namba nne wa mwaka 2014 ambao pamoja na sheria na nyaraka nyingine na miongozo inayohusu elimu ulilenga katika kuhakikisha kuwa vitabu vya ziada na kiada vinavyotumika katika shule zote zilizosajiliwa nchini
āVitabu vinatumika ni vyenye maudhui yanayoendana na mila ,desturi na utamaduni wa nchi yetu na kuweza kumlinda mtoto wa kitanzania aliyepo shuleni.āamesema na kuongeza kuwa
āKatika kusimamia utekelezaji wa waraka huu,wizara imebaini kuwa kuna baadhi ya shule ambazo zimekuwa zikiingiza na kutumia vitabu ambavyo maudhui yake yanakinzana na mila,desturi ,miongozo pamoja na tamaduni za kitanzania ambapo maudhui hayo yanahatarisha ukuaji na malezi ya watoto na pia kupotosha mila na desturi za nchi yetu.ā
Amesema vitabu hivyo visivyoruhusiwa orodha yake itatangazwa na Waziri wa Wizara hiyo Profresa Adolf Mkenda pamoja na kuweka zuio la matumizi ya vitabu hivyo.

More Stories
Twange:Miradi ya Umeme Dar kukamilika hivi karibuni
Mwanasheria Mkuu asisitiza ushahidi wa kidijitali katika mashauri
Vijana warejea darasani Tabora