December 27, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Wanafunzi tisa wadaiwa kujinyonga hadi kufa

Na Esther Macha,TimesMajira Online. Mbeya

WANAFUNZI wa kike watano kutoka shule tofauti tofauti wanadaiwa kujinyonga hadi kufa kwa kipindi cha miezi tisa mkoani Mbeya.

Kamada wa Polisi Mkoa wa Mbeya Kamishna Maidizi Mwandamizi wa Jeshi la Polisi, Ulrich Matei amesema kuwa matukio hayo yametokea Wilaya za Mbarali, Kyela na Mbeya mjini.

Kamanda Matei ametoa taarifa hiyo ya wanafunzi kujinyonga kwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Albert Chalamila alipokutana na wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya kutwa ya Kyela.

Kamanda Matei amesema shule hiyo, inatajwa kuwa ndiyo kinara kwa wanafunzi kujinyonga kwani ndani ya mwaka huu, tayari wanafunzi watatu wa shule hiyo wamejinyonga hadi kufa.

Mkuu wa Wilaya ya Kyela, Claudia Kitta amesema baada ya matukio hayo ya wanafunzi kujinyonga kukithiri, Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya imelazimika kuchukua hatua za makusudi.