Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online DSM
WANAFUNZI wa darasa la tatu wa shule ya msingi St Anne Marie Academy wamemshangaza Kamishna wa elimu nchini, Dk. Lyabwene Mutahabwa kwa namna wanavyomudu lugha ya kingereza na kifaransa.
Wanafunzi hao walionyesha umahiri wao wakati wa mahafali ya 15 ya kidato cha sita ambapo mmoja alikuwa akizungumza Kifaransa na mmoja kutafsiri kwa lugha ya Kingereza.
Kamishna huyo ameelezea kufurahishwa kwake na umahiri wa wanafunzi hao huku akipongeza uwekezaji mkubwa uliofanywa na shule hiyo jambo ambalo linasaidia jitihada za serikali.
Mkurugenzi wa shule za St Anne Marie Academy, Dk. Jasson Rweikiza amesema wanafunzi wote watakaopata daraja la kwanza atawazawadiwa simu janja macho matatu.
Amesema kwa namna wanafunzi hao walivyoandaliwa na kupata matokeo mazuri kwenye mitihani ya majaribio ana mayumaini kwamba asilimia kubwa watapata daraja la kwanza.
“Nimeahidi iphone macho matatu lakini kutokana na namna mlivyoandaliwa nimeanza kuwa na wasiwasi nkwamba iwapo wote mtapata Division I nitapata wapi fedha za kuwanunulia iphone nyinyi wote,” amesema
Amesema matokeo mazuri ya shule hiyo yanatokana na mazingira mazuri ya kusomea ikiwemo chakula kizuri, maji ya uhakika na umeme na maktaba za kisasa.
Amesema shule imeendelea kuhakikisha inakuwa na madarasa bora nay a kutosha ili darasa likae na wanafunzi wachache kumwezesha mwalimu kumiliki darasa vizuri ili wanafunzi wamwelewe.
Amesema shule hiyo ina maktaba nzuri iliyosheheni vitabu vingi vya kiada na ziada na mazingira safi ya kusomea kama viyoyozi na huduma ya afya ya uhakika kwa wanafunzi.
Amesema shule imeendelea kujiimarisha zaidi na imeweka uzio eneo lote la shule na ina askari wa kutosha wenye mafunzo na uwezo wa kutumia silaha za moto pamoja na mbwa wakali kwaajili ya ulinzi wa shule.
Amesema kutokana na sababu za kuwepo kwa majanga ya moto kwenye maeneo mbalimbali shule imechukua tahadhari ya kujikinga na ajali zitokanazo na moto kwa kuweka vifaa vya kuzimia moto.
Dk. Rweikiza ameiomba serikali kuwapunguzia kodi wamiliki wa shule ambao alisema wanalipa kodi 18 hali inayofanya kiwango cha ada kuwa juu hivyo kuwabebesha mzigo wazazi.
Amesema iwapo kodi hiyo ingepungua huenda ada nayo ingeshuka hivyo kuwapunguzia mzigo wazazi na kwamba kupungua kwa ada kungesababisha wanafunzi wengi kupata elimu.
“Kodi ni nyingi sana michango Manispaa Kata, kodi za moto na leseni mbalimbali tunaomba ziangaliwe kwa maana ya kumpunguzia mzigo wazazi,” amesema
Dk. Rweikiza amerudia ahadi yake kwamba hakuna mwanafunzi wa shule zake ambaye atafukuzwa shule iwapo atafiwa na wazazi akiwa anasoma kwenye shule hizo.
“Hii ni ahadi yangu ya muda mrefu na narudia tena mwanafunzi yeyote ambaye atafiwa na mzazi akiwa kwenye shule hizi hatafukuzwa shule, awe shule ya awali, msingi au sekondari ataendelea kusoma hadi amalize,” amesema Dk. Rweikiza.
Kwenye hotuba yake, Kamishna wa Elimu, Dk. Mutahabwa ameipongeza shule hiyo kwa namna ambavyo imekuwa ikifanya vizuri kwenye mitihani yake ya kitaifa.
Amempongeza Mkurugenzi wa shule hizo, Dk. Rweikiza kwa uwekezaji mkubwa alioufanya kwenye elimu na kwamba amekuwa msaada mkubwa kwa serikali ya awamu ya sita.
Ameelezea kufurahishwa na umahiri ulioonyeshwa na wanafunzi kwenye lugha ya Kiswahili na Kingereza na kuwataka walimu wa shule hiyo wasibweteke na badala yake waendelee kufundisha kwa bidii.
More Stories
TASHICO,yatoa ufafanuzi Mv.Serengeti kutitia upande mmoja
TAG yampongeza Rais Samia
CCM Tabora yamfariji mjane wa kada anayedaiwa kujiua