January 11, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Wanafunzi nchini wahimizwa kusoma masomo ya sayansi

Na Lubango Mleka, Timesmajira Online.

WANAFUNZI nchini hapa wametakiwa kuchangamkia fursa ya kusoma masomo ya sayansi ili kuweza kupata wataalamu wengi kwani Serikali imeboresha miundombinu ya elimu inayokwenda sambamba na tekinolojia.

Hayo yamebainishwa na Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake CCM (UWT) Taifa na MNEC Zainab Shomari katika ziara yake aliyoifanya Kata ya Bukoko Jimbo la Igunga ya kukagua utekelezaji wa miradi ya ujenzi wa shule ya sekondari Bukoko na zahanati ya Ipumbulya ambapo amewataka wanafunzi katika shule hiyo kusoma masomo ya sayansi ili kupata wataalamu mbalimbali watakao kwenda sambamba na sayansi na teknolojia.

Makamu Mwenyekiti UWT Taifa na MNEC Zainab Shomari akitoa pongezi kwa Mkuu wa Wilaya ya Igunga Sauda Mtondoo katikati na Mwalimu Mkuu wa shule ya sekondari Bukoko Mary Peter Malaba wa kwanza kushoto kwa kusimamia kikamilifu ujenzi wa maabara,jengo la utawala na nyumba za walimu shuleni hapo.

“Ninawaomba wanafunzi wote msome kwa bidii kwani nimeambiwa Mkoa wa Tabora katika matokeo ya mwaka huu mmefanya vizuri sana, hivyo niwasisitize kusoma masomo ya sayansi ili tupate wataalamu wengi kwani serikali inatoa fedha nyingi kuboresha elimu, nimeona mmejengewa maabara nzuri sana ya masomo ya sayansi, jengo zuri la utawala na nyumba za walimu myatunze majengo haya, pia nitoe wito kwa wazazi kushirikiana na walimu kufuatilia maendelo ya watoto hawa,” amesema Shomari.

Aidha MNEC Shomari amekagua zahanati ya Ipumbulya ambayo ilipokea kiasi cha shilingi milioni 50 za ukamilishaji wa boma na miundombinu yake ambapo ameridhishwa na ujenzi huo.

Makamu Mwenyekiti UWT taifa MNEC Zainab Shomari akikagua maktaba katika shule ya sekondari ya Bukoko.