Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online DSM
WANAFUNZI wa Shule ya Msingi Green Acres, wamewapagawisha wazazi na wageni waalikwa kwenye mahafali yao baada ya kuzungumza kwa ufasaha lugha ya Kifaransa na Kichina.
Hayo yamejiri leo kwenye mahafali ya 23 ya shule hiyo Mbezi Beach Salasala, wakati wanafunzi hao wakionyesha maonyesho mbalimbali kwa wageni waalikwa na wazazi wao.
Wanafunzi hao wameonyesha umahiri huo kwa kuzungumza mambo mbalimbali kwa lugha hiyo kwa ufasaha huku wanafunzi wengine wakitafsiri kwa lugha ya kingereza hali iliyoibua shangwe.
Mmoja wa wazazi aliyefika kwenye mahafali hayo, Vick Minja ambaye mwanaye anahitimu darasa la saba amewapongeza walimu wa shule hiyo kwa kujiongeza na kuamua kuwafundisha wanafunzi hao lugha za kichina na Kifaransa.
Amesema kwa dunia ya sasa mtu kuwa na uwezo wa kuzungumza lugha ya kingereza na kifarasa ni sifa ya ziara ya kupata kazi hivyo alisema kuna haja kwa shule zingine kuiga mfano kama huo.
“Wachina wanapatikana kote duniani na taifa lao linazidi kukua kiuchumi kwa hiyo mwanafunzi akijua kichina uwezekano wa kupata kazi ni mkubwa kwasababu wachina wanazidi kuja Afrika kuwekeza kwenye miradi mbalimbali,” amesema
Mkuu wa shule hiyo, Minani Kafugugu, amesema waliamua kuanza kuwafundisha wanafunzi wa shule hiyo lugha ya kichina baada ya kuona ni lugha ambayo inaendelea kuhitajika zaidi duniani.
Amesema kuna umuhimu kwa shule mbalimbali kufundisha lugha za kifaransa na kichina kwani mtu kufahamu lugha zaidi ya moja kunampa uhakika wa kupata ajira kulinganisha na wasiojua lugha hizo.
Amesema mbali na lugha hizo kitaaaluma shule hiyo iko vizuri na kwamba mwaka huu wanatarajia kupata matokeo makubwa kwenye mitihani ya darasa la saba.
Amesema wamekuwa wakipata matokeo makubwa kitaaluma kwenye mitihani ya kuanzia darasa la nne, la saba, kidato cha pili na cha nne na kwmba hayo yanatokana na kuajiri walimu wenye weledi , wanaojituma na wenye nidhamu ya kazi yao.
Wakati huo huo, wanafunzi wa shule hiyo wameonyesha vipaji vya aina yake kwenye michezo mbalimbali waliyoonyesha kwenye mahafali hayo.
Wanafunzi hao walionyesha umahiri wa hali ya juu kwenye kucheza na kuimba nyimbo mbalimbali za bongo fleva hali iliyowaamsha wazazi kwenda kuwatunza kwa zawadi mbalimbali.
Mmoja wa wazazi, James Mloka amepongeza walimu wa shule hiyo kwa kuibua vipaji vya wanafunzi hao kwani kuna umuhimu wa wanafunzi kujifunza viytu zaidi mbali ya masomo ya darasani.
“Binafsi nimefurahi sana kuona wanafunzi wana vipaji vya aina hii nani muhimu shule zingine ziige kwa Green Acres kwasababu wanafunzi wanaweza kuwa na vipaji lakini visipoibuliwa wanaweza kubaki kama walivyo kwa hiyo kuwe na program ya kuibua vipaji kama ilivyo hapa,”amesema
More Stories
Mpango ashiriki mazishi ya Mama yake Serukamba
TRA kuongeza idadi ya waendesha uchumi walioidhinishwa
TRA Tanga wajivunia ukusanyaji mapato