October 6, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Wanafunzi Chuo cha Ustawi kushiriki Hult Prize Kenya

Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online

Kupitia wazo Lao la kibishara na kibunifu linalohusu “Recycling of plastic waste into eco-brick “ (Utengenezaji na uzalishaji wa tofali kwa kutumia taka za plastiki) wanafunzi watatu kutoka #chuochaustawiwajamii ni Miongoni mwa wanafunzi kutoka vyuo mbali mbali Duniani wanaokutana Jijini Nairobi Nchini Kenya Kuwania Tuzo hii.

Tuzo ya Hult ni shindano kubwa zaidi la ujasiriamali wa kijamii kwa wanafunzi duniani, Inayoendeshwa kwa ushirikiano na Umoja wa Mataifa na timu za wanafunzi kutoka vyuo vikuu mbalimbali duniani.

Mashindano haya yanalenga kutatua tatizo la kijamii lenye umuhimu kwa kuanzisha biashara ya kijamii inayoweza kukua na kudumu. Washindi wa mwisho watawasilisha miradi yao mbele ya jopo la majaji mashuhuri, viongozi wa biashara duniani, viongozi wa mawazo, na watetezi wa mabadiliko ili kushinda dola milioni 1 za Marekani na kuanzisha biashara zao.

Mkuu wa #chuochaustawiwajamii Dkt. Joyce Nyoni tarehe 04/06/2024 ameongea na wanafunzi hao ambao ni Hellena Sailas, Maria Daudi, na Method Dallu ambao tarehe 05/06/2024 waliwasili Jijini Nairobi tayari kwa Shindano hilo.

Dkt. Joyce amewapongeza sana Wanafunzi hao wabunifu wa #ISW na kuwapa Mkono wa Kheri na kuwatakia Mafanikio katika Ushiriki wao.