Na Rose Itono,TimesMajira Online, Dar
WANAFUNZi wabunifu wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere wamesema mafunzo ya uongozi na maadili wanayopewa chuoni hapo yamewajenga kuwa imara katika shughuli zao za baadaye
Wakizungumza kwenye Maonesho ya 16 ya Elimu ya Juu ya Sayansi na Teknolojia yaliyofanyika kwenye viwanja vya mnazi mmoja,ya walisema mafunzo ya uongozi na maadili wanayopewa yamewawezesha kuwa imara katika utekelezaji wa shughuli zao mbalimbali zikiwemo bunifu
.
Jonas Katial mmoja wa wanafunzi aliyehitimu diploma ya TEHAMA chuoni hapo amesema ameamua kubuni mfumo utakaomuwezesha mkulima kumwagilia
shamba bila kuwepo ili kumpunguzia muda wa kukaa shambani pasipo kufanya shughuli nyingine za kujiongezea kipato.
Amesema kwa kutumia mfumo huu mkulima atakuwa anapata taarifa zote za umwagiliaji zinazoendelea shambani kupitia simu yake ya mkononi.
“Mfumo huu wa umwagiliaji unajiongoza wenyewe baada ya kupima udongo, udongo ukiwa mkavu pampu inawaka yenyewe
na kuanza kumwagilia shamba na wakati huo kitendo hicho kinapoendelea mkulima atapata ujumbe wa kumtaarifu kuwa shamba lake linamwagiliwa, “amesema Katial na kuongeza kuwa mara udongo utakaoloa maji ya kutosha mkulima atapata taarifa na pia
mfumo huu wa umwagiliaji haubagui chanzo cha maji na ni rahisi kuutumia.
More Stories
Amos Lengael Nnko afariki kwa ajali ya gari
Gridi za Tanzania, Kenya kuimarisha upatikanaji wa umeme
Mama Zainab:Watoto yatima ni jukumu la jamii yote