January 23, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Bw. Hosea Kashimba (kushoto) akimuhudumia mwanachama wa Mfuko huo aliyetembelea banda la Muko katika maonesho ya 44 ya biashara ya kimataifa ya Dar es Salaam kwenye viwanja vya Julius Nyerere maarufu Sabasaba Julai 10, 2020. Katikati ni Afisa Habari Mkuu wa PSSSF, Bw. Abdul Njaidi.

Wanachama 826 wa PSSSF wamehudumiwa kufikia Julai 10 Maonesho ya Sabasaba

Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online, Sabasaba

MKURUGENZI Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumisi wa Umma (PSSSF) CPA. Hosea  Kashimba amesema zaidi ya wanachama wapatao 826 wamehudumiwa na PSSSF kwenye maonesho ya 44 ya biashara ya kimataifa ya Dar es Salaam tangu yalipoanza Julai 1 hadi leo Julai 10, 2020.

Kashimba (kushoto) na Njaidi (mwenye t-shirt ya blue) wakibadiliahsna mawazo na baadhi ya wakurugenzi wa NSSF kwenye banda la ushirikiano namba 13 ambalo mifuko hiyo miwili inashirikiana.

Kashimba ameyasema hayo leo Julai 10, 2020 wakati alipotembelea viwanja vya Julius Nyerere maarufu Sabasaba barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam ambako ndiko kunakofanyika maonesho hayo yaliyopewa kauli mbiu isemayo “Viwanda kwa Ajira na Biashara Endelevu.

“Tuko katika banda namba 13 tuliloliandaa kwa ushirikiano na NSSSF kwa lengo la kutoa huduma bora kwa wanachama wetu, tunatarajia tutaendelea kuwahudumia wanachama zaidi hadi hapo maonesho yatakapofikia kilele chake, tunawakaribisha wanachama wetu na wananchi kwa ujumla. Hapa sabasaba tuna ofisi kamili .” Amesema Kashimba.

Kashimba akiwa katika picha ya pamoja na kikosi kazi cha PSSSF kinachoendelea kuwahudumia wanachama wa Mfuko huo kwenye banda namba 13 maonesho ya 44 ya biashara ya kimataifa Sabasaba

Amesema huduma zote zinazotolewa kwenye ofisi za PSSSF zilizoeneo nchi nzima zinapatikana kwenye banda hilo na kuwahimiza wanachama na wananchi kufika ili wahudumiwe.

“Mwanachama atapata huduma zote kama anataka kupata ufafanuzi kuhusiana na uanachama wake, kuhakiki taarifa zake, kuangalia michango yake na mambo yote yanayohusiana na uanachama huduma zinapatikana hapa.” Alisisitiza.

Wanachama wakiwa kwenye banda la PSSSF
Meneja wa PSSSF Mkoa wa Ilala, Uphoo Swai (kulia) akifurahi na mwanachama wa Mfuko Malima Ndelema wakati akimuhudumia kwenye banda la Mfuko.
Meneja wa PSSSF Mkoa wa Kinondoni, Ritha Ngallo (kushoto) akimuhudumia mwanachama