January 23, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Wanaanchi waaswa kutumia teknolojia katika kilimo ili kuonmngeza mnyororo wa thamani

Na Joyce Kasiki,Timesmajira online,Mbeya

MKUU  wa kitengo cha masoko na Uhusiano wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo vijijini, Godrick Ngoli amesema kuwa wanatamani  kuona wananchi wanatumia kilimo cha kiteknolojia katika kuwaletea Maendeleo na  watumie kilimo kama biashara kwa kuongeza mnyororo wa thamani katika mazao yao.

Pia amewasa wananchi na wakulima kutembelea banda la Chuo hicho lililopo ndani ya banda la Wizara ya Fedha na Mipango katika maonesho ya wakulima na wafugaji maarufu nane nane yanayoendelea kwenye viwanja vya John Mwakangale ambapo kitaifa yanafanyika mkoani Mbeya.

Akizungimza katika maonesho ya mkoani Mbeya  Ngoli amesema lengo la wananchi na wakulima hao kwenda kutembelea banda hili ni kubadilishana uzoefu ili waone ni kwa namna gani wanaweza kuongeza thamani katika shughuli za Uvuvi, Ufugaji na kilimo.

Amesema kuwa shughuli hizo kuu tatu zinafanywa na kila Matanzania aliyoko mjini na vijijini huku akisema mfumo wa maisha umebadilika tofauti na awali kilimo kilikuwa vijijini.

” Tunataka tuachane na ule  Uvuvi wa kutegemea bahari, maziwa na mito tuende kwenye Uvuvi wa mabwawa ya kuchimba na sisi kama chuo cha Mipango tuna wataalamu katika sekta hii na tuna uzoefu wa muda mrefu,” amesema Ngoli.

Amesema, awali walikuwa na mradi huo ambao ulifadhiliwa na serikali ya Europe Union ambao ulikuwa katika Mkoa wa Dodoma ukishirikisha vijiji vinne ambapo waliwajengea uwezo wananchi katika maeneo kame na waliweza kufuga samaki.

Naye Afisa Mipango wa Chuo hicho Francis Mbonde amewahamashisha wananchi kujiandaa na zoezi la kuhesabiwa katika Sensa ya Watu na Makazi inayotarijiwa kufanyika Agosti 23 mwaka huu.

Amesema jambo hilo ni muhimu Serikali ina nia njema ya kutaka kujua idadi ya watu pamoja na makundi mbalimbali, mahitaji yao katika kuendesha shughuli zao na Taifa kwa ujumla.

” Tuna wasisitiza wananchi kuweza kujiandaa na zoezi hili ambalo ni muhimu kujua mahitaji ya watu, idadi ya watu ili kupanga mipango ya nchi. Kwa sisi chuo cha Mipango tunapenda kuwakaribisha watu, vikundi, Taasisi za serikali waje kujiunga na chuo chetu ili kujijengea uwezo katika nyanja ya kuandaa mipango ya Taasisi zao,Idara zao, vikundi vya tutawapatia mafunzo ya kuandaa mipango yao  pamoja na bajeti,” ameeleza Mbonde.

Awali Afisa Masoko na Uhusiano  wa Chuo hicho Nuru Joseph amesema  wapo katika maonesho hayo ambayo kitaifa yanafanyika mkoani Mbeya yenye kaulimbiu  inavyosema “Agenda 10/30, Kilimo  ni Biashara Shiriki Kuhesabiwa kwa mipango bora ya Maendeleo ya  kilimo, mifugo na uvuvi,”.

Amesema kuwa chuo hicho pia kinashiriki maonesho hayo Kanda ya Kati Dodoma hivyo anawakaribisha wananchi kutembelea banda lao lililopo katika jengo la Wizara ya Fedha na Mipango ili waweze kuona kozi mbalimbali zinazotolewa na chuo hicho