November 6, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Wana Ilala watakiwa kushikamana

Na Heri Shaaban, TimesMajira Online, Ilala

Diwani wa Kata ya Ilala ambaye pia ni Mjumbe wa Baraza Kuu CCM Taifa,Saady Kimji, amewataka wana Ilala kuacha siasa chafu badala yake wametakiwa kushikamana kuwa wamoja kujenga chama na Serikali katika kusimamia miradi ya Maendeleo .

Diwani Kimji aliyasema hayo katika mkutano wa hadhara CCM Mivinjeni wakati wa kikao cha kumshukuru mdau wa Maendeleo Pamoja na kumpongeza , Juma Kibondei , ambaye aneshirikiana na uongozi wa Kata ya Ilala kuondoa Mafuriko Mtaa wa Mivinjeni Ilala .

“Wana Ilala wezangu sasa tufanyeni kazi tuwe wamoja katika kukisaidia chama na Serikali katika kuleta maendeleo tuache kufanya siasa chafu sio Maendeleo ” alisema Kimji .

Diwani Kimji aliwataka waache makundi Ilala hayawezi kuleta maendeleo badala yake washikamane kuwa wa moja katika kutekeleza Ilani ya chaama cha Mapinduzi CCM katika kumsaidia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan.

Alisema yeye Diwani wa Ilala ataendelea kuchapa kazi kuwatumikia wana Ilala ndani ya chama na serikali ametaka washirikiane katika kuleta Maendeleo ya Wananchi na kusimamia miradi ya Maendeleo ya serikali na ndani ya chama na jumuiya kubuni miradi ya kujikwamua kiuchumi .

Akizungumzia Maendeleo ya Ilala alisema katika sekta ya Elimu Msimbazi sekondari wamejenga madarasa manne,Sekondari ya Mivinjeni wamejenga kwa fedha za COVID ,Elimu Msingi shule ya Msingi Boma Serikali imejenga madarasa mawili mikakati ya Serikali kupata madarasa mapya Saba.

Alisema kwa sasa wanatarajia kujenga darasa la Elimu ya awali,Jengo la Utawala ,Vyoo vya walimu na wanafunzi na darasa Maalum la watu wenye Ulemavu ambapo mpaka sasa Shilingi milioni 365 zimeshaelekezwa mikakati iliyopo kutafuta Mkandarasi .

Akizungumzia sekta ya afya alisema kata ya Ilala sasa wanajenga zahanati ya Kata ambayo itakuwa inatoa Huduma za Mama na Mtoto inajengwa na wadau wa Maendeleo wametafutwa na Mbunge wa Jimbo la Ilala Mussa Zungu kwa ushirikiano wa ofisi yake ya Diwani .

“Zahanati ya Ilala ikikamilika itakuwa mkombozi kwa Wananchi wa Ilala ambao awali walikuwa wakipata huduma Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Amana
kwa sasa imepewa hadhi ni Hospitali kubwa “alisema .