Na Esther Macha,TimesmajiraOnline,Mbeya
HALMASHAURI ya Wilaya ya Chunya mkoani Mbeya imesema asilimia 95 ya vijiji vilivyopo katika halmashauri ya wilaya hiyo vinapata huduma za afya baada ya Serikali kutoa fedha kwa ajili ya kuboresha miundombinu kwa maeneo ya Pembezoni.
Tamimu Kambona ni Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Wilaya ya Chunya amesema hayo wakati wa kuwasilisha taarifa kuhusu utekelezaji mafanikio ya miaka mitatu ya Rais Samia Suluhu Hassan kwa msemaji mkuu wa serikali.
Kambona amesema kwamba Serikali imetoa sh.Bil.6 kwa ajili ya kuboresha shughuli za afya pamoja na ukarabati wa vituko vya afya , hospitali ya Wilaya na zahanati.
“Zaidi ya Bil.6 tumetunia katika kipindi hiki cha miaka mitatu tukianzia hospitali ya wilaya katika hospitali yetu ambapo zaidi ya Bil.3 tumetunia ikiwemo ujenzi na upanuzi wa hospitali ambapo awali ilikuwa inaonekana kama kituo cha afya na Sasa imeshakiwa hospitali kamili ya wilaya na zaidi ya majengo nane yanajengwa baada ya kupata fedha kutoka kwa Mh .Rais Dkt Samia Suluhu Hassan”amesema Mkurugenzi huyo.
Hata hivyo Kambona amesema kuwa wawemeza kujenga vituko vya afya vitano wilayani humo na pia wamejenga kituo cha afya kimoja kwa kutumia mapato ya ndani ya halmashauri ambapo wametumia Mi.466 kwa kata ya Sangambi na tayari kinafanya kazi.
Kambona amesema kuwa mafanikio kwa kipindi cha miaka mitatu halmashauri haijawahi na jengo la utawala lilokuwa linatumiwa na halmashauri kama jengo la utawala hivyo wamemshukuru Rais Dkt Samia kwa kuwapatia zaidi ya Bil.1.4 ,ambazo zilikusanywa kwenye mapato ya ndani na kuanza ujenzi na kukamilika na kuhamia kwenye jengo hilo jipya.
Kwa upande wake Msemaji mkuu wa serikali,Mabhore Matinyi ameshukuru kazi kubwa iliyofanywa na halmashauri za mkoa wa Mbeya ikiwemo halmashauri ya Wilaya ya Chunya.
“Wakurugenzi mshirikishe vyombo vya habari katika kuzungumzia miradi ya halmashauri iliyotekelezwa kwa kipindi cha miaka mitatu ili wananchi waweze kupata taarifa zizohusu miradi “amesema.
More Stories
TAG yampongeza Rais Samia
CCM Tabora yamfariji mjane wa kada anayedaiwa kujiua
FDH yaanza kutekeleza mradi wa kuwajengea uwezo wanawake wenye ulemavu