Judith Ferdinand, Timesmajira Online, Mwanza
Onyo limetolewa kwa wamiliki wa vyombo vya moto wanoruhusu vyombo vyao kuingia barabarani huku vikiwa havijakatiwa bima.
Onyo hilo limetolewa leo Agosti 24, 2023 na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza SACP Wilbrod Mutafungwa wakati wa kikao na waendeshaji wa vyombo vya moto na viongozi wao,Latra, TARURA, TANROAD,Ofisa Mipango Miji pamoja na wadau wengine wa usalama barabarani jijini Mwanza.
Mutafungwa amesema baadhi ya wamiliki wa vyombo vya moto wamekuwa hawakati bima kwenye vyombo vyao hali inayosababisha usumbufu kwa madereva wao pindi zinapotokea ajali.
Hivyo ametumia fursa hiyo kumuagiza Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Mwanza (RTO) Sunday Ibrahim na timu yake kutengeneza utaratibu wa kukagua bima kwenye magari na vyombo vingine vya moto.
“Endapo ikibainika chombo chochote cha moto kinachotakiwa kuwa na bima na hakijakatiwa bima mmiliki apelekwe mahakamani,”
Huku akitamtaka pia kuchukua hatua kali za kisheria kwa madereva wote wanaokatisha njia nyakati za jioni.
More Stories
Ilemela yatenga milioni 920 kwa ajili ya mikopo ya vikundi
Tabora Network yawezesha vijana kiuchumi
Wanawake watakiwa kutochafuana kuelekea uchaguzi mkuu