Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online
Wamiliki wa fremu na majengo ya biashara mkoani Arusha wametakiwa kulipa kodi ya zuio ya asilimia 10 badala ya kuliacha jukumu hilo mikononi mwa wapangaji jambo ambalo limetajwa kukwamisha ustawi wa biashara zao kwa kuwafanya walipe kodi mara mbili.
Awali akizungumza wakati akitoa ripoti ya mwenendo wa kampeni ya elimu ya kodi ya Mlango kwa Mlango inayoendeshwa na maafisa wa mamlaka hiyo,Meneja wa TRA Mkoa wa Arusha Eva Raphael anabainisha kero inayokumba wafanyabiashara ikiwemo wamiliki wa nyumba kukwepa kodi hiyo na kulazimisha wapangaji kulipa jambo ambalo ni kinyume cha sheria.
Kufuatia changamoto hiyo mkuu wa mkoa wa Arusha John Mongela anatoa maelekezo kwa wafanyabiashara ikiwemo wamiliki wa majengo kulipa kodi kwa mujibu wa sheria, ili kuunga mkono Serikali katika sekta mbalimbali za kimaendeleo.
Nao baadhi ya wafanyabiashara waliofikiwa na Kampeni hiyo wameishukuru mamlaka ya mapato kwa kutoa elimu kwa wafanyabiashara pamoja na kusikiliza kero mbalimbali zinazo wakabili.
More Stories
AZAKI yawasilisha mapendekezo yao kwa Serikali katika kuboresha Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050
CP.Wakilyamba :Uvamizi maeneo ya hifadhi ya taifa katavi haukubaliki
Watu wawili wanaodhaniwa majambazi wapigwa risasi na Polisi