Na Joyce Kasiki, Timesmajira Online, Dodoma
KATIBU Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii,Jinsia na Makundi Maalum Dkt.Zainab Chaula amelitaka Shirikisho la Umoja wa wamachinga (SHIUMA) kote nchini kutokubali kutumika kwa namna yoyote ile na badala yake watumie fursa ya amani na utulivu kufanya shughuli zao za kujitafutia kipato.
Dkt.Chaula ameyasema hayo leo wakati akifungua mkutano wa shirikisho la wamachinga nchini ambao umewakutanisha na viongozi wa Wizara kwa lengo la kujadiliana namna wanavyoweza kufanya shughuli na kuhakikisha wanakuza mitaji yao lakini pia kukuza uchumi wa nchi.
“Rais alipokutana na wamachinga alisema kwamba wamachinga ni kundi maalum na kulipeleka kwenye Wizara ya Maendeleo ya Jamii,Jinsia na Makundi Maalum ,nasi tunashukuru kupewa jukumu hili sasa tunahitaji kukaa pamoja na kuzungumza mambo mbalimbali yakiwemo changamoto zinazowakabili wamachinga ili tutazitatue kwa pamoja.”amesema Dkt.Chaula
Amelitaka kundi hilo kufanya kazi kwa kushirikiana na kupendana badala ya kuwekeana chuki vitu ambavyo vinaweza kusababisha kukata mitaji yao.
More Stories
Waziri Mavunde:Benki Kuu yanunua tani 2.6 za Dhahabu nchini
Kampeni msaada wa kisheria ya mama Samia kutatua kero za kisheria Katavi
Wizara ya madini yakusanya bil.521 nusu ya kwanza mwaka wa fedha 2024/25