Na maureen paul, TimesMajira Online
Mgomo ulioibuka siku ya jumatatu Juni 20 nchini zimbambwe ambapo Madaktari, Wauguzi walianzisha mgomo huo kutokana kuwa mzozo wa kiuchumi wa hivi sasa umesababisha kutokua na thamani yeyote ya fedha.
Wauguzi nchini humo wanalipwa dola 18,000 za zimbambwe ambazo ni sawa na dola 55 za kimarekani kulingana na soko la ubadilishanaji fedha hivi sasa huku mshahara wa walimu unasemekana kuanzia dola 75 kwa mwezi.
Wafanyakazi wa afya walikusanyika nje ya ofisi za bodi ya kitaifa ya afya,iliyopo kwenye mojawapo ya hospital kubwa zaidi nchini zimbabwe.
Askari wa utulivu wa ghasia waliitwa karibuni na eneo hilo wakati wagonjwa hospitalini wakiachwa bila huduma zozote.kiongozi wa shirika la wauguzi la zimbambwe Enock Dongo amesema kuwa bodi ya afya pamoja na wizara ya afya wamekataa kusikiliza maoni na madai yao.
Wiki iliyopita serikali nchini humo ilisema kwamba ingeongaza maradufu mishahara ya wafanyakazi wote wa serikalini,lakini Enock Dongo kiongozi wa shirika la wauguzi la zimbambwe amesema kwamba kufikia sasa hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa.
Source VOA
 Â
More Stories
Kapinga atoa maagizo TANESCO ,kuhusu Vijiji vinavyolipia gharama ya mijini kuunganisha umeme
Ukiukaji wa Uhuru wa Kidini na Kutovumiliana Huzusha Malumbano ya Kimataifa
NLD kipo tayari kwa uchaguzi wa Serikali za Mitaa