Na Heri Shaaban,TimesMajira Online,Iringa
OFISI ya Rais Tawala za Mikoa (TAMISEMI )yatoa agizo kwa Walimu wapya ambao wanatakiwa kuripoti kazini Julai mwaka huu mwisho Julai 14/2021 nchi nzima
Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu TAMISEMI Profesa Riziki Shemdoe wakati wa ziara ya kikazi katika Manispaa ya Iringa kuangalia ujenzi wa madarasa mapya na mabweni.
“Serikali mwaka huu sekta ya Walimu wameipa kipaumbele ili vijana wetu waweze kupata elimu bora tumeajili Walimu tunaomba wale wote waliopata ajira mwaka huu mwisho kufika Julai 14 mikoa yote ,nje na hapo nafasi zao zitazibwa na Walimu wengine “amesema Profesa Shemdoe
Profesa Shemdoe ameagiza walimu wote kulipoti katika vituo vyao vya kazi walivyopangiwa kwa wakati pamoja na watumishi wapya ili waweze kutekeleza majukumu yao.
Akizungumzia maendeleo ya Iringa wakati wa kukagua mabweni ya wanafunzi na madarasa mapya katika shule ya Serikal iliyogharimu shilingi milioni 700 Profesa Shemdoe alimpongeza katibu Tawala Mkoa Happiness Seneda na Mkurugenzi wa halmashauri ya Iringa Hamid Njovu katika usimamizi mzuri kusimamia miradi ya Serikali.
Amewataka wakurugenzi wengine kuiga mfano huo katika usimamiaji fedha za Serikali zitumike kama ilivyokusudiwa na kazi iliyopangwa .
More Stories
Rais Samia afurahia usimamizi mzuri wa miradi
Rais Samia apongezwa kwa kuboresha huduma kwa wazee
Watu 5,000 kuhudhuria tamasha la utamaduni Songea