Na Stephen Noel Mpwapwa.
Mkuu wa wilaya ya Mpwapwa Mkoani Dodoma Bi Sophia Mfaume Kizigo ametoa amri kwa maafisa Elimu wote ndani ya wilaya hiyo kuhakikisha shule zote za Msingi na sekondari zinakuwa na walimu walezi kwa lengo la kupunguza vitendo vya ukatili kwa watoto wawapo shuleni.
Mkuu wa wilaya hiyo ametoa agizo hilo kwenye mkutano wa Siku moja uliondaliwa na Asasi ya kiraia jukwaa la utu wa mtoto CDF iliyo kutanisha Wadau wote wanao fanya afua za kumlinda mtoto na kujali ustawi wa mtoto.
Amesema Ili kuhakikisha watoto wanakuwa Kwenye mazingira ya usalama na watu wanao ratibu kero zinazo wakabili watoto au pindi wafanyiwapo ukatili nyumban au eneo la Shule.
“Sasa naagiza kwa maafisa Elimu wote Msingi na sekondari kuwa ifikapo kesho shule zote ziwe na matron na Patron hili halihitaji mpango kazi lifanyiwe kazi mala moja” aliongea Dc Kizigo.
Kaimu Ofisa Elimu sekondari bwana Ally Akida amesema Kwa Sasa Mpwapwa Ina Shule 33 za sekondari ambazo jumla ya wanafunzi 17249 na wanafunzi walio panga vyumba ( mageto) ni wanafunzi 1204 ambao hujilea wenyewe na wapo Katika hatari kubwa ya kufanyiwa ukatili kutokana na mazingira wanayo ishi.
Afisa Elimu Msingi Bwana Jackson Mpankuli alisema kuhakikisha watoto wanakuwa Katika usalama ni jukumu wazazi,/ walezi na walimu wanashirikiana Katika malezi ya watoto wao na wanafunzi wawapo shuleni.
Ofisa wa dawati WP 2420 Ditektivu Sanjeti Magreth alisema kuanzia mwezi March jumla makosa 15 ya ubakaji yalilipotiwa katika kituo cha polisi wakati makosa matano ya ulawiti yalilipotiwa na makosa mawili ya kuwapa wanafunzi mimba pia yalilipotiwa kutoka mwezi March 2023 na alisema yapo katika hatua mbali mbali za kimaamuzi katika vyombo vya kisheria.
Kwa upande Wake mkurugenzi mtendaji wa jukwaa la utu wa mtoto Koshuma Mtengeti alisema tangu shirika hili lianze kufanya kazi katika wilaya hiyo mwaka 2017 wamefanikiwa kupunguza vitendo vya ukatili wa Kijinsia kwa Jamii kwa ikiwemo watoto wa kike pia amesema wameongeza uelewa kwa jamii ambapo umesababisha taarifa za vitendo vya ukatili kulipotiwa Katika vyombo vya kutoa maamuzi.
More Stories
Zaidi ya wananchi 32,000 Vijiji vya Wilaya za Morogoro na Mvomero kuanza kupata mawasiliano
Wafanyabiashara waomba elimu ya namna watakavyorejea soko kuu
DCEA,Vyombo vya Ulinzi na Usalama vyafanya operesheni ya kihistoria