November 7, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Walimu wa saikolojia watumika kufundisha watoto

Na Esther Macha , Timesmajira Online,Mbeya

Shule ya Holyland iliyopo katika Mji mdogo wa Makongolosi wilayani Chunya mkoani Mbeya inawatumia walimu wa saikolojia kwa watoto ambao wanaonekana kuwa na changamoto ya kutoelewa na wenye kukosa raha wakati wa ufundishaji wa masomo darasani .

Akizungumza na Timesmajira ofisini kwake , Mkurugenzi wa Shule hiyo ,Lawena Nsonda (Baba Mzazi)amesema kuwa kitu cha utofauti katika shule hiyo kuwa walimu wakiona mwanafunzi haelewi darasani wanamtumia mwalimu wa Saikolojia ambaye kazi yake ni kuangalia matatizo ya watoto.

Mwalimu huyo ambaye anakaa na kujenga nao urafiki ambao husaidia kuwa huru kueleza changamoto na matatizo yao ambapo wapo wanaoishi na mama wa kambo au baba wa kambo wamekuwa wakiwapa mateso wanapo. kuwa nyumbani hali inayosababisha kushindwa kuelewa wanapokuwa darasani.

“Kutokana na changamoto wanazokutana nazo tunachofanya ni kujenga urafiki na watoto hawa kisha kuwasaidia kupitia walimu wa saikolojia, “amesema.

Nsonda amesema kuwa kuna mtoto alillkuwa akifundishwa pekee yake lakini alikuwa haelewi hivyo ilibidi kuchumkua mwalimu wa saikolojia ambaye alimfanyia maombi mtoto huyo na akadai kuwa aligundulika kuwa alikuwa na hirizi kiunoni.

Kwa mujibu wa Nsoda ameeleza kuwa baada ya wazazi wa mtoto huyo kuitwa walidai kuwa alikuwa anaishi na bibi yake na mtoto kueleza kuwa walikuwa wanapaa angani na bibi yake .

Aidha Mkurugenzi huyo amesema kwamba hivi sasa mtoto huyo anashika namba moja darasani ambaye awali alikuwa

“Pia watoto wanafundishwa kulingana hali halisi ya dunia inakoelekea wasiangalie baadhi ya tamthilia pamoja na baadhi ya katuni zisizo na maadili,”.

Mwalimu wa Saikolojia katika shule hiyo Ezekiel George,amesema kuwa mambo anayofanya katika kuwaweka sawa watoto shuleni hapo ni pamoja na kuhakikisha watoto hawapati changamoto za kijamii na kidini.

“Ninapoona mtoto hayupo kwenye mazingira ambayo yanamfanya kukosa raha namfanyia ushauri nasaha ili kumuweka sawa na kurudi katika hali yake ya kawaida,nina uzoefu na watoto wenye changamoto hizi tunahitaji kuwasaidia sana na wanarudi vizuri na kuwa vizuri kimasomo,”amesema.

John Kulwa ni mkazi wa Makongolosi wilayani Chunya amesema watoto katika shule wanalelewa kiroho kwani hata mtoto akienda shuleni hapo akiwa tofauti na wenzie baada ya muda anawakuwa sawa na watoto aliowakuta.