December 25, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Walimu wa dini watakiwa kuzingatia makuzi ya watoto ili kuwaepusha na mmomonyoko wa maadili

Na Daud Magesa, Timesmajira Online, Mwanza

OFISA Elimu Mkoa wa Mwanza,Martin Nkwabi amesema wanahitajika walimu
wanaofundisha watoto masomo ya dini wanaozangatia malezi na makuzi yao ili kuwaepusha na mmmomonyoko wa maadili.

Ametoa kauli hiyo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza,Said Mtanda wakati
akifunga sherehe za kukaribisha mwaka mpya wa Kiislamu 1446 Hirjiria.

Nkwabi amesema shule nyingi zinachangia kuporomosha utu wa mtu haziwabadilishiwatoto na kuwafanya wakue katika maadili,ili kumaliza tatizo la mmomonyoko wa maadili vipindi vya dini vifundishwe na walimu wanaozingatia makuzi ya watoto hao,si wale wasio wa maadili.

“Mafunzo ya dini yakifundishwa na walimu wanaozingatia makuzi na maleziya watoto yatakuwa silaha ya kuondoa tatizo hilo la maadili,hivyo tuone namna ya kuimarisha elimu ya dini pia makuzi na malezi nyumbani familia zisaidie kuongeza thamani ya watoto na hili waislamu mnafanya vizuri,”amesema.

Pia amesema wazazi walio wengi hawawezi kufuatilia mafundisho na masomo ya watoto wao shuleni kubaini kama wanafika shuleni au la,
bahati mbaya wanawapeleka shule bila kuwa na malengo mahususi watoto wasome ili wawe madaktari,walimu au wataalamu katika kada tofauti.

“Wazazi wengi hawafuatilii mafundisho ya watoto shuleni kama
wanavyofuatilia mashamba kuona mazao yao yana hali gani vinginevyo watapata
hasara,bahati mbaya wanawapeleka shule bila malengo,tukiimarisha ngazi ya
watoto tutakuwa na kizazi na taifa la maadili,”amesema.

Nkwambi amewapongeza BAKWATA kwa kujenga watu (waumini) wenye uwezo wa
kutawala mazingira yao ikiwemo elimu ya kutambua saratani ya shingo ya kizazi,fistula,kupanda miti na kuchangia damu.

“Binafsi nisigekuwa na maadili ningefanya kazi ninayoifanya au ningefanya uharibifu,tusaidieni kutengeneza watoto wenye maadili waje kutusaidia,wazazi baadhi hawachukulii uzito kuwapa elimu watoto,tuwekeze katika elimu ya watoto wetu,”amesema.

Sheikh wa Mkoa wa Mwanza,Alhaji Hassani Kabeke amesema wamejipanga
kufanya maendeleo kwa kujenga vituo vya afya saba mkoani humo,hivyo katika kila
shughuli ya kiislamu kutakuwa na changizo la maendeleo kwa hiari bila kumkwaza
mtu.

Sheikh Kabeke amewataka waislamu wasishsindwe kuchangia maendeleo kwa
kukatishwa tamaa na maneno ya watu wazingatie kauli mbiu ya “BAKWATA mpango mzima kwa maendeleo,BAKWATA Mwanza jenga hospitali,bidhaa tano BAKWATA inshaallah tutajenga hospitali,”.

Awali Katibu wa BAKWATA Mkoa wa Mwanza,Ustaadhi Ramadhan Chanila amesema mpango wa miaka mitano wa maendeleo una vipaumbele sita vya kila msikiti kuchangia sh.5000 kwa mwezi,Baraza la Maulid,viwanja na misikiti itakayofanyika shughuli
ya kiislamu asilimia 20 itachangia maendeleo huku Ahlul Khayr (Watu wenye Heri) 10,000 wakichangia sh. 1000 na kuendelea.

Amesema BAKWATA mkoani humu imeadhimisha mwaka mpya wa 1446 kwa kupanda miti 175,000 ili kutunza mazingira,kutoa elimu ya saratani ya shingo ya kizazi,fistula,kuchangia
damu,kutembelea mradi JUVIKIBA wa ufugaji samaki kwa vizimba na kuendelesha michuano ya kombe la Mutfi 2024.