November 6, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Walimu masomo ya sayansi wametakiwa kuwalea vizuri na kuwavumilia watoto

Na Esther Macha, Timesmajira, Online, Masasi

WALIMU wanaofundisha masomo ya sayansi katika Halmashauri ya Mji wa Masasi mkoani Mtwara wametakiwa kuwalea vizuri na kuwavumilia watoto wanaowafundisha masomo hayo ili wayapende na kuja kuwa na wanasayansi bora.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mtendaji Mji wa Masasi , Erica Yegella wakati akizungumza na walimu 126 wa masomo ya sayansi ambao wanapatiwa mafunzo endelevu kazini ili waweze kufundisha watoto kwa ufanisi .

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mji Masasi,Erica Yegella akizungumza na walimu wa masomo ya sayansi wa halmashauri hiyo katika shule mpya ya Mkomaindo ambao wanapatiwa mafunzo ya elimu endelevu kazini.

‘’Niwaombee heri katika siku hizi mbili za mafunzo yenu ,mimi huwa naheshimu sana walimu wa shule za msingi kwasababu yeye ndiye msingi kuanzia awali ,msingi mpaka darasa la saba nyie dira ya maisha maana nyie ndo mnatoa viongozi ,wakurugenzi ,mkuu wa wa wilaya , mwalimu bora,”amesema na kuongeza kuwa

“Nina hakika mtakuwa walimu bora na si bora mwalimu ufanisi wenu na ubunifu wenu na utendaji kazi katika kufundisha watoto wetu bila kuogopa masomo nautegemea sana ‘’amesema Mkurugenzi huyo .

Aidha Mkurugenzi Yegella amesema kuwa walimu wa masomo ya sayansi ni lulu inapaswa kutunzwa na kwamba mkusanyiko huo ni neema na kwamba Hamlashauri ya Mji wa Masasi ipo kwenye mkakati wa kuboresha elimu na kuwa wapo mjini lakini ufaulu si mzuri wanawashinda Newala Vijijini ambao hawana hata umeme .

Ofisa limu msingi mji Masasi ,Hamida Msemwa akitoa maelezo kwa mkurugenzi mtendaji Erica Yegella kuhusu Mafunzo hayo kwa walimu

‘’Lakini kutokana na hilo mmenipa mtihani wa kutathimini hili suala namna gani ya kuboresha na kuendeleza masomo ya sayansi mkumbuke katika elimu sekondari tunatengeneza maabara ya masomo ya sayansi sasa tusipokuwa na wanasayansi tutakwama na mkumbuke katika lugha ya mawasiliano ya kimataifa ni kingereza tusipojua lugha hiyo tutakwama”amesema na kuongeza kuwa

“Tusipojua hisabati tutakwama maisha yote tukilala tukiamka ni hisabati tukipumua ni sayansi , kwa hiyo nyinyi mnasoma masomo ya binadamu kila siku nyie ni watu muhimu sana kwani ndio maisha ya kila siku ya kila mmoja wetu”amesema.

Ofisa elimu Msingi Halmasahauri Mji Masasi Hamida Msemwa,amesema kuwa mafunzo hayo wamegawa katika masomo matatu ambayo ni sayansi,hisabati na kiingereza yamekuwa ni changamoto ya muda mrefu shuleni hivyo kupitia mafunzo endelevu kwa walimu kazini yamekuwa msaada mkubwa kwa walimu .

Hata hivyo Msemwa amesema kuwa katika Halmashauri Mji wa Masasi kuna shule 44 zikiwemo shule za binafsi tatu na za serikali 41 na wote wameshiriki katika mafunzo hayo na hakuna aliyebaguliwa hivyo kila shule ina wawakilishi watatu kwa masomo yote na kwamba shule mpya ya Mkomaindo ikikamilika idadi ya shule itafika 45.

Baadhi ya walimu kati ya 126 kutoka Shule mbalimbali katika Halmashauri wa Mji Masasi

Mwalimu wa shule ya msingi Machombe, Sitty Ntile amesema mafunzo hayo yatawajengea uwezo mkubwa katika kufikisha maarifa kwa watoto kwani masonmo ya sayansi yamekuwa hayafanyi vizuri kutokana na ugumu wake.

Kama inavyoelezwa na baadhi ya watoto kuwa masomo hayo ni magumu hivyo ni vema serikali iwe inafanya masomo hayo mara kwa mara ili kuweza kuwajengea uwezo zaidi.

‘’Masomo haya hayafanyi vizuri sana kama tunavyoelewa wengi wetu wamekuwa wakisema kuwa haya masomo yamekuja na meli mara ndege hivyo ni masomo ambayo yana ugumu kiasi fulani,‘’amesema.