Na George Mwigulu,Timesmajiraonline,Katavi.
MKUU wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko,amewataka Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi wa Halmashauri na walimu wakuu wa shule za msingi kuimarisha programu za chakula shuleni ifikapo Januari 2025 kwani ni daraja la mafanikio kwa wanafunzi.
Programu ya chakula shuleni inatajwa kumpa kila mtoto matumaini ya kujifunza na motisha ya kusalia shuleni na humpa afya kupitia lishe bora inayoruhusu kujifunza na kufanya vyema kwenye masomo yao hivyo kupanua wigo wa fursa za kielimu.
Akizungumza na Wanahabari Disemba 23, 2024 wakati akitoa salamu za siku kuu ya Chrismas na Mwaka mpya amebainisha kutoa ruhusa kwa shule kufanya vikao na wazazi na walezi kukubaliana namna ya kuchangia chakula cha wanafunzi.
Akiwa katika ofisi yake, Mrindoko ameweka wazi ifikapo Januari 13, 2025 wakati muhula wa masomo unapofunguliwa program ya chakula shuleni kuanza kutekelezwa kwa kila shule za mkoa huo.
Mbali na kutoa wito huo,amesisitiza wazazi na walezi kufanya maandalizi mapema ya watoto wao pindi shule zinapofunguliwa wahakikishe wanaripoti kwa wakati.
Mrindoko amesema maandalizi ya wanafunzi 13,887 waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza katika shule za sekondari yako tayari kwani wanaongezeko la vyumba vya madarasa 28 kati ya mahitaji ya nyumba 283 na kufikia jumla ya vyumba vya madarasa 311 huku suala la madawati likiimarishwa zaidi.
Hata hivyo kiongozi huyo wa mkoa wa Katavi,amesema Hajalidhishwa na uandikishaji wa wanafunzi wa darasa la awali na darasa la kwanza wa asilimia 34.4 ambapo ili kufikia malengo makubwa amewaomba wazazi na walezi kuendelea kuwaandikisha watoto.
Ametoa rai kwa viongozi wa serikali za mitaa kuhakikisha wanakwenda kwa kila nyumba za mitaa, vijijini na vitongoji kufanya ufuatiliaji wa watoto wanaositahili kuandikishwa shule.
Shule za mkoa wa Katavi zinatarajia kufunguliwa Januari 13, 2025 huku ikitarajiwa kuwa na ongezeko kubwa la wanafunzi wanaaonza shule ya msingi ambapo serikali imeweka mikakati madhubuti sio ya kuwapokea wanafunzi hao pekee bali na wale wanaonza elimu ya sekondari kwa kuimarisha kila miundombuni itakayowezeha mazingira rafiki ya kujifunzia.
More Stories
Serikali kupeleka mawasiliano maeneo ya mipakaniÂ
Sekondari ya Butata mbioni kufunguliwa Musoma Vijijini
TIC yapongeza mradi wa Kampuni ya Big Best