Na Penina Malundo,Timesmajira
WAKUU wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) wametoa maazimio yakumaliza mgogoro wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo leo jijini Dar es Salaam.
Miongoni mwa maazimio hayo ni pamoja kuagiza wakuu wa majeshi wa nchi za Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika kukutana ndani ya siku tano na kuchukua hatua za kusitisha mapigano bila masharti, kuandaa mpango wa usalama kwa mji wa Goma na kufungua uwanja wa ndege wa mji wa Goma.
Akisoma maazimio hayo leo Februari 8,2025 jijini Dar es Salaam,Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Veronica Muen Nduva, amesema maazimio mengine yaliyotolewa na viongozi hao ni pamoja na kusitisha mapigano hayo kwa haraka na kufanya mazungumzo ya moja kwa moja, ambayo yatahusisha pia wanajeshi na wasio wanajeshi, ikiwa ni pamoja na kundi la M23 na Mengine ni kuondolewa kwa vikosi vya kigeni visivyoalikwa ndani ya DRC.
Amesema pia wameazimia kurejesha kwa haraka huduma za kijamii ikiwemo uzikaji wa miili ya watu waliofariki na kuwapatia matibabu watu waliopata majeraha.”Wakuu hao wameazimia kwa pamoja na kuwataka mawaziri wa nchi za EAC/SADC kukutana ndani ya siku 30 kujadili na kutoa mrejesho wa kile kilichoamuliwa na wakuu wa majeshi kuhusu kusitisha mapigano DRC-Congo.
Amesema pia wakuu hao wameazimia kuwepo kwa majadiliano ya mara moja kila mwaka ili kufanya tathmini ya mzozo huo na kuwaalika viongozi wa Afrika Mashariki kila mwaka kupitia masuala hayo ya DRC”imeeleza taarifa ya wakuu wa nchi za SADC,EAC.
Aidha katika maazimio hayo,wakuu hao wamethibitisha kuendeleza mshikamano na kujitolea kuendelea kuiunga mkono DRC na kuhakikisha inapata uhuru wa eneo lake.
More Stories
Wanafunzi wawili waliodaiwa kutekwa wapatikana,watuhumiwa wauwawa
Watumishi Madini waaswa kufanya kazi kwa bidii, kuwa wazalendo
Masauni:Biashara ya Kaboni ni Ukombozi kwa Taifa