Esther Macha,Timesmajira,Online,Mbeya
NAIBU Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar Dkt.Mohammed Said Mohammed amewaagiza Wakuu wa Mikoa ya Mbeya na Songwe kuhakikisha wanafuatilia
utekelezaji wa miradi ya maendeleo iliyoelekezwa na Rais Samia Suluhu Hassan.
Huku akiwataka Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kwenda kwa wananchi kueleza mambo makubwa yaliyofanywa na serikali ya awamu yasita sambamba na kuwachukulia hatua watu wanaokwamisha utekelezaji wake.
Dkt, Mohammed ameyaeleza hayo mkoani hapa ikiwa ni siku ya kumpongeza Rias Samia Suluhu Hassan kwa kutimia miaka miwii ya uongozi wake tangu alipopokea kijiti baada ya kufariki aliyekuwa Rais wa awamu ya tano Dkt.John Magufuli mwaka 2021.
Amesema kila kiongozi ana wajibu wa kueleza mambo yote muhimu yaliyofanywa na CCM pamoja na serikali yake kwani mambo mengi ya muhimu yamefanywa.
” Serikali  imeleta fedha nyingi za miradi ya maendeleo siyo ziwekwe mifukoni hapana imeleta ili zijenge miundombinu na isaidie sisi na wananchi wote ni imani yangu kuwa ile hospitali ya Mama na Mtoto itaweza kusaidia mpaka wenzetu wa nchi za jirani hivyo tutumie nafasi zetu kuelezea vipaumbele ambavyo tumepewa mimi naamini baada ya miaka mitatu ilani yetu hii tutakuwa tumeimaliza na kuwarudishia na chenji wanaMbeya’’amesema.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Mbeya ,Dkt. Stepheni Mwakajumulo amesema kuwa Mkoa huo umetulia kwa muda mfupi miradi mingi ya kimaendeleao imezinduliwa.
Dkt. Mwakajumulo amesema kuwa mafanikio ya awamu ya sita ni pamoja na kutatua mgogoro wa Mbarali ambao ulikuwa ni ugonjwa mkubwa uliosumbua kwa muda mrefu karibu miaka 10 na ulipelekea kutofanya siasa zisizo na afya kwa miaka miwili mgogoro umeisha na kubaki historia.
‘’Sisi tupo pamoja kutekeleza ilani ya CCM ndiyo maana hata vyama vya upinzani wanakosa sababu ya kuzungumza kutokana na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi kuwa pamoja’’amesema.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Mbeya , Juma Homera amesema kuwa mkoa umepokea bilioni 1.6 kwa ajili ya ujenzi wa vyuo vya ufundi stadi(VETA)katika Wilaya ya Mbarali na Chunya kwa lengo la kuwawezesha vijana kujiajiri .
‘’Serikali ya Mama Samia imetoa zaidi ya bil.34 kwa ajili ya kuboresha miundombinu katika uwanja wa kimataifa Songwe(SIA) ambapo ndege kubwa aina ya Aier Bus zinatarajia kuanza kutua mkoani hapa’’amesema Homera.
More Stories
Mpango ashiriki mazishi ya Mama yake Serukamba
TRA kuongeza idadi ya waendesha uchumi walioidhinishwa
TRA Tanga wajivunia ukusanyaji mapato