Na Mwandishi Wetu,Timesmajira
Wakulima wa Mkoa wa Tabora wameishukuru Serikali ya Awamu ya 6 inayoongozwa na Rais, Dkt. Samia Suluh Hassan kutokana na usimamizi wake madhubuti katika kuiwezesha Kampuni ya Mbolea ya Tanzania (TFC) kujikita katika usambazaji na kuuza mbolea za ruzuku kwa wingi na kuwafikia wakulima kwa wakati.
Shukrani hizo zimetolewa mwishoni mwa wiki hii na wakulima hao mkoani Tabora wakati timu ya wana Habari kwa kushirikiana na Maofisa wa (TFC), waliowatembelea wakulima hao kwa ajili ya kutoa El;imu ya matumizi bora ya mbelea pamoja na kuona faida ya kutumia mbolea zinazosambazwa na (TFC), na jinsi zinavyowanufahisha wakulima katika kilimo chao pamoja na kuona wanazopata wakulima hao.
Aidha, Wakulima hao waliotembelewa na Timu hiyo inatokana na kuonekana kukidhi ubora katika soko tangu waanze kutumia mbolea za ruzuku zinazosambazwa na Kampuni ya (TFC), katika Mazao ya Tumbaku, Mpunga, Mahindi, Mboga mboga Nyanya, Pili pili Hoho, Vitunguu na mazao mengine ya Matunda kama vile Matikiti maji.
Akizungumza na wakulima hao, Afisa Kilimo Mwandamizi kutoka Bodi ya Tumbaku Sostenes Kikwelele amesema kuwa katika soko wanapokea Mitumba 650, kwa siku ya Tumbaku kutoka Chama cha Msingi Usindi AMCOS ambapo Mitumba hiyo imesibitishwa kuwa na viwango bora vinavyohitajika katika soko la dunia na kuwa na vigezo v inavyotakuwa pia wanatalajiwa kupata bei nzuri katika uuzaji wa Tumbaku zao.
“Tofauti na awali wakulima walikuwa na changamoto ya upatikanaji wa mbolea na kusabisha uchelewaji wa matumizi na kusababisha kuvuna Tumbaku kidogo iliyo chini ya viwango, lakini tangu kuanza kutumia Mbolea kutoka Kampuni ya (TFC), msimu huu wakulima wengi wamepata Tumbaku ambayo imekidhi vigezo kwa madaraja tofauti”,amesema Afisa huyo.

Kwa upande wake, Joaqium Herman ambaye ni Mwenyekiti wa Chama cha Msingi Usindi kilichopo wilayani Kaliua, ametoa ushuhuda wake kwa kusema kuwa awali mazao yao yalikuwa siyo bora kama sasa hivi kutokana na kuanza kutumia matumizi ya mbolea za aina ya NPK 12, 18 24 na CAN zinazosambazwa na kuuzwa na Kampuni ya ( TFC).
Herman,amesema kuwa Tangu kuanza kutumia Mbolea za (TFC) kilimo cha Tumbaku kimekuwa na tija hususani ilipofikia kwenye zoezi la uchomaji wa Tumbaku ambapo awamu hii haikuweza kuoza na imekuwa nzito yenye rangi inayovutia sokoni kutokana na matumizi ya mbolea kutoka (TFC).
“Wakulima kwa kweli wamefurahi kutokana na matumizi ya mbolea hiyo ya (TFC) na hata kama kuna ukame kama mwaka Jana, mbolea hii ukipanda tena inashika na kustawi vizuri”, amesema Herman.

Mwenyekiti huyo,amesema kuwa Mbolea zote kuanzia NPK 12, 18 24 na CAN kwenye USINDI AMCOS hakuna mkulima aliyekosa mbolea ya aina yoyote kwa kuwa mbolea zote zilifika kwa wakati kuanzia ya kupandia hadi na ya kukuzia.
Herman, ameendelea kueleza kuwa kutokana na ubora wa mbolea za kutoka (TFC), msimu huu wakulima wengi wamepata Tumbaku zenye ubora wa daraja la kwanza na pili kwa kiwango kikubwa.
Daniel Mwakienda Mkulima wa kilimo cha mbogamboga cha kabichi kutoka Kijiji cha Mabama, amesema kuwa awali alikuwa anatumia mbolea nyingi kwenye kupandia tofauti na mbolea ya TFC nilikuwa napata mazao kidogo.
Mwakienda, amesema kwa sasa ana vuna Kabichi nyingi na zenye ubora kwa kuwa anatumia mbolea ya Dampo kutoka (TFC), ambayo inadaiwa kushika kwa haraka kwenye udongo wa kupandia na unatumia mbolea kidogo na kupunguza gharama ya maisha tofauti na hapo awali ilikuwa unatumia gharama kubwa katika kununua mbolea.
“lakini kwa sasa matumizi ya fedha yamekuwa ya chini mno na kufikia kiasi kingine cha fedha, natumia kwenye matumizi mengine ya kifamilia na hasiti kusema kuwa mbolea kutoka (TFC), Imebadilisha maisha yangu na familia inayonizunguka”,amesema mkulima huyo.
Mwakienda, akizungumizia kuhusu upatikanaji wa mbolea kutoka (TFC) amesema kuwa upatikanaji wa mbolea hizo ni rahisi sana na zinapatikana tena kwa wakati na muda mwafaka tofauti na awali upatikanaji unakuwa mgumu na unaifuata mbali na kuchelewa kazi za shambani.
Naye, Abass Jummane, mkazi wa Kijiji cha Kipela na mkulima wa Bustani na mazao ya mengine amesema kuwa mbolea za (TFC), ni bora nyakati zote tangu alipoanza kutumia Mbolea hizo kuanzia Dampo na Urea na kufanya kilimo kuwa rahisi tofauti na awali.
Jumanne amesema kuwa hapo awali alikuwa na mafanikio madogo kutokana na kutumia Mbolea ambazo hazina ubora, lakini tangu kampuni ya Serikali (TFC) ilipoanza kusambaza mbolea yao, imekuwa na tija na sasa naweza kutumia mbolea kidogo na kupata mpunga mwingi kutokana na ubora wa mbolea za kutoka (TFC).
“kipindi anatumia mbolea tofauti na za kutoka (TFC), alikuwa akipata tabu sana kutokana na kwanza kutafuta mbolea na hata mavuno yanakuwa tofauti na matarajio, lakini tangu kuanza kutumia mbolea ya (TFC), analima Heka Moja na kupata Mpunga Gunia 20 mpaka 25, huku Mahindi akipata ya kutosha.
More Stories
RC Senyamule:Jamii Cup siyo burudani tu,ni chombo cha malezi
Benki ya Equity yawakutanisha wawekezaji,Wafanyabiashara kutoka nchi mbalimbali kujadili masuala ya uwekezaji
Kongamano la kimataifa la kusoma Qur’an kufanyika Mei 24,2025