January 23, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Wakulima nyanda za juu kusini waaswa kutumia mbegu za Mahindi aina ya Pannar na Pioneer.

Na David John, Timesmajira Online, Mbeya

AFISA kilimo kutoka kampuni ya Corteva Agri Science yenye makao makuu yake jijini Arusha charles Fungameza amewataka wananchi wa Nyanda za juu kusini hususani katika mikoa ya Mbeya ,Njombe ,Iringa kufika katika maonyesho ya kitaifa ya nanenane ili kuweza kupata mbegu zilizobora na zenye kuleta tija kwenye uzalishaji wa mazao.

Akizungumza na waandishi wa habari Agosti 6 mwaka huu katika banda la Corteva lilipo kwenye viwanja hivyo amesema kuwa wao kama corteva wana aina mbili za mbegu za Mahindi ambazo ni Pannar na Pioneer nakwamba mbegu hizo zinafanya vizuri sana na zinaleta tija kwa mkulima katika uzalishaji .



Fungameza amesema kuwa wana mbegu za pannar za kati na muda mrefu lakini wanambegu za pioneer za muda wa kati,muda mrefu na wachini na mbegu hizo katika nyanda za juu kusini zinafanya vizuri sana kwani kuna mvua za kutosha na baridi hivyo zinavumilia hali ya hewa ya ubaridi.

Amefafanua kuwa kuna mbegu zinaitwa pana 691 ambayo mkulima akipanda kwa hekari moja anauwezo wakuvuna gunia 35 mpaka gunia 40 kwani zinavumilia hali ya hewa ya baridi na mvua na zinakuwa na tija katika kipato.



“Mbegu hizi katika maeneo haya ya ukanda wa nyanda za juu kusini zinavumilia sana sababu kuna baridi kali na mvua nyingi lakini mbegu zetu za Pannar na Pioneer zinavumilia hali ya hewa hii ya baridi na zinamavuna ya kutosha kwa mfano kuna mbegu zinaitwa pannar 691 kwa hekari mkulima akipanda anavuna gunia 35 mpaka 40 ukizingatia pamoja na kuvumilia vua nyingi na baridi ,kuoza nma magonjwa yatokanayo na majani lakini bado yanakupa uhakika wa mavuno.”amesema Fungameza



Nakuongeza kuwa “Hivyo hivyo kwaupande wa pioneer 3812w, 30G-19 nazo zinavumilia sana ukanda huu nazinakupa mazao ya uhakika kwahiyo mbegu zinapatikana kwa urahisi hivyo mkulima akipanda mbegu zetu licha kuwa bei zinaweza kuwa ghari lakini atapata malipo ya bei kwa kuvuna mazao mengi.



Ameongeza kuwa bidhaa ambazo zinatoka kwenye kampuni ya Corteva ni kampuni ambayo imejikita sana kwenye ubora na inajua inachokifanya hivyo waje wapite kwenye banda lao ili kujifuza namna wanavyowahudumiwa wateja na wakitoka hapo baada ya kuaza msimu lazima watakuwa na sehemu ya kuazia ,na kwamba watapanda mbegu kwao ama mafunzo hivyo watakuwa na uhakika wakupata sehemu sahihi ya mbegu.