Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online
MUDA mfupi baada ya jana Kamati ya Utendaji ya klabu ya Yanga kutangaza kumsimamisha kazi Kaimu Katibu Mkuu wake ambaye pia ni Mkurugenzi wa Sheria na Wanachama, wakili Simon Patrick kwa tuhuma za kuihujumu klabu hiyo, mwenyewe amefunguka na kudai kuwa kamwe hawezi kufanya kitu chochote cha kuihujumu klabu hiyo kutokana na kiapo cha maadili ya taaluma yake.
Minong’ono ya bosi huyo kutimuliwa Yanga ilianza kusikika toka wiki iliyopita lakini hakuna kiongozi yeyote aliyekuwa tayari kulitolea ufafanuzi suala hilo.
Lakini taarifa kutoka ndani ya klabu hiyo zilidai, kiongozi huyo anatajwa kuihujumu timu hiyo kwa kutoa siri na lizipeleka kwa ‘Mahasimu wao’ jambo ambalo linaweza kukwamisha mikakati yao ya kutwaa ubingwa wa msimu huu wa Ligi Kuu Tanzania Bara (VPL).
Pia inasemekana kuwa, kuanzia sasa majukumu ya Wakili Patrick yatakuwa chini ya Mwenyekiti wa klabu hiyo Dkt. Mshindo Msolla.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana na Mwenyekiti wa klabu hiyo, Dkt. Mshindo Msolla imeweka wazi kuwa wameamua kufikia maamuzi hayo baada ya kikao cha dharura cha Kamati ya Utendaji kilichokaa jana Novemba 17, 2020 ambacho kilifanyika maalum kwa ajili ya kusikiliza shutuma ambazo amehusishwa nazo.
“Kwa dhumuni la kuhakikisha haki inatendeka, Kamati ya Utendaji itateua Kamati Huru kuchunguza swala hili na kutoa maamuzi yenye tija kwa pande zote hivyo, Kamati ya Utendaji itaisubiri Kamati Huru kukamilisha uchunguzi wake na kutoa ripoti juu ya tuhuma hizi,” alieleza Dkt. Msolla katika taarifa yake.
Lakini muda mfupi baada ya klabu hiyo kuweka wazi maamuzi yake, Wakili Patrick amefunguka na kufafanua tuhuma ambazo zilielekezwa juu yake na kudai kuwa kamwe hawezi kufanya jambo lolote la kuihujumu klabu ambayo ni kama dini kwake.
Katika ufafanuzi wake, aliouita ‘Taarifa yangu binafsi hukusu hujuma klabuni’ waliki huyo amefafanua mambo mbalimbali ikiwemo
Vikao vya siri na Kiongozi wa maasimu
“Nakiri kukutana na mtendaji mwenye rank kama ya kwangu kama alivyomtaja maeneo ya Yatch Club lakini sio vikao vya siri kwani kilichonikutanisha na mtendaji huyo ni swala la muhimu ambalo viongozi wangu wakubwa watatu walikuwa wanajuwa na walinipa baraka zote, na mara baada ya kikao hicho nilirudisha mrejesho wa kilichonipeleka na hii tunaongelea tarehe 20/10/2020 hivyo hakuna siri yoyote”
“Yatch Club mimi ni Visiting Member, ni sehemu ya wazi ambapo huwa napenda kupumzika. Kama ingekua nina jambo la siri kuna sehemu kibao ningeweza kufanya bila mtu yoyote kujua, am too smart for that. Kwenye hili pia mjue sisi ni maasimu wetu kuna sehemu uhitajiana kikazi na kama kuna jambo ambalo linatuumiza huweka itikadi zetu pembeni na kuungana kutafuta suruhu kiutendaji na hili halijaanza jana.
Nahofia nafasi yangu kuchukuliwa na Senzo
“Mimi nakaimu nafasi ya Katibu Mkuu kwa muda lakini nimeajiriwa kama Mkurugenzi wa sheria, hivyo basi siwezi kumuhofia Mr. Senzo kwani yeye sio Mwanasheria bali ni Mshauri mkuu wa Klabu, Kukaimu nafasi maana yake unashikiria kwa muda viongozi wanaweza kupiga simu moja tu kwamba kuanzia leo sio tena kaimu . nikatii hofu sijui inatoka wapi”.
Nimehujumu kesi ya Morrison
“Mimi ndiye niliyetengeneza ule mkataba, so kisheria nilikua sifudhu kutetea ile kesi, hivyo basi Klabu iliamua kuweka wanasheria wabobezi wawili ambao wamenizidi seniority kuweza kupambana na hiyo kesi na ndio wanaotuwakilisha huko CAS, na niseme ukweli kwa experience yao sina wasiwasi hata mmoja kuhusu hiyo case ya CAS. Case yetu CAS itnesafiliwa kwa namba CAS2020/A/7397.1tii maana yake ni kesi ya 7397 na ikumbukwe CAS inapokea kesi kutoka nchi ambazo ni wanachama wa FIFA dunia nzima, na ina kesi nyingi sana kama ilivyo mahakama ya rufaa ya Tanzania, hivyo msiwe na haraka sana kwenye maswala ya kisheria”.
Mimi kufuta kesi ya Morrison TFF
“Mpaka sasahivi Yanga ina Case zake 4 ambazo shirikisho limeamua kuzipotezea, Kesi ya Kabwili, kesi ya Morrison kuhongwa $5000 kushawishiwa kuihama Yanga, Pingamizi la usajili wa Morrison na Kesi ya Mkataba wa Morrison ambao haujasainiwa na pande zote mbili, nina ushahidi wa kujitosheleza kwamba hizi kesi bado zipo pending kwenye shirikisho letu tukufu.
Pia akiongelela lile la kutopokea simu za Mwenyekiti, Wakili huyo amesema, hawezi kulitolea ufafanuzi jambo hilo Mwenyekiti ndiye mtu anayeongoza kwa kuwasiliana nae zaidi ya wengine na kudai kuwa kwa nafasi yake kama angekua mtu wa kuihujumu klabu basi angekuwa milionea.
More Stories
Othman awakabidhi jezi Zanzibar Heroes
Rais Samia: Yanga endeleeni kuipeperusha bendera ya Tanzania
15 wajinoa Juventus,akiwemo mtoto wa Mwenyekiti wa CCM Mbeya