March 7, 2026

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Wakazi Segera,Wadau wa Mazingira waungana kuadhimisha siku ya usafi Duniani

Na Penina Malundo,Timesmajira

WAKAZI wa Kijiji cha Segera Wilayani Handeni Mkoani Tanga, kwa kushirikiana na Wadau wa Mazingira kutoka mashirika ya Umma na binafsi pamoja na makampuni ikiwemo Zalongwa Technologies, Bigman Security, Mkulago Memorial, TEPA Tanzania, John Kijazi Bus Stendi Waste Peakers Korogwe, wameungana kuadhimisha Siku ya Usafi Duniani kwa kufanya usafi katika eneo la Mji wa Segera “Kituo cha Usafi cha Segera Roundabout” kilichoanzishwa mwaka 2021 Mkoani Tanga.

Akizungumza leo Wilayani humo, Mratibu wa Siku ya Usafi Duniani Wilayani Handeni Mkoani Tanga, Bw. Abdallah Lungo, alisema zaidi ya washiriki 128 waliweza kujitokeza wingi katika Madhimisho hayo kwa kufanya usafi kwa pamoja katika Eneo la Mita 250 zilizopo Katika Kata ya Segeara, Kijiji cha Segera.

Amesema wadau hao wameungana kwa lengo la kupambana na uchafuzi wa Mazingira hususani Taka za Plastiki zinazotupwa katika maeneo ya umma ikiwemo katika vyanzo vya maji na kwenye mifereji ya barabara.

Lungo amesema kuna umuhimu wa utunzaji wa mazingira na kuhakikisha maeneo yanakuwa safi muda wote,hivyo kupitia maadhimisho hayo yanawafanya kuwakumbusha umuhimu huo na kutafakari namna ya uchafu wa mazingira unavyoathiri jamii.

”Siku ya leo ni maalum kwaajili ya usafi duniani,hivyo kama wadau wa usafi kutoka mashirika mbalimbali Pamoja na Wananchi wa Kijiji cha Segera tumeungana katika kuadhimisha siku hii ambayo ilianza tangu mwaka 2018.

”Mwaka huu 2025 tumekuwa tukihamasisha masuala ya usafi huku tukisindikizwa na kauli mbiu ”Dunia inaadhimia kufikia asilimia 5 ya watu wote duniani katika shughulia usafi hususan kudhibiti taka ngumu na kuangalia namna gani jamii inaweza kushiriki na kuondoa tatizo la Taka,”amesema

Amesema kila mwaka maadhimisho hayo ufanyika Septemba 20 na kwa mkoa wa Tanga wameweza kuadhimisha katika mji huo na kuungwa mkono na mashirika Pamoja na kampuni 11 katika kuweka eneo hilo.

”Miongoni mwa mashirika hayo ni Pamoja na Zalongwa Technologies,Nipe Fagio,Bigman Security, Ruvu Environmental Cleaning and Conservation,LATRACCC, Segera Secondari,John Kijazi Bus Stand Waste Peakers and TEEA ambao wameonesha nia ya kuungana kw pamoja katika kuadhimisha siku hiyo,”amesema,

Kwa upande wake Mratibu wa Taasisi ya Nipe Fagio Mkoa wa Tanga, Paulo Sarakikya amesema siku ya usafi duniani ilianzishwa mwaka 2018 lengo likiwa ni kuhamasisha jamii kwenye zoezi la usafishaji wa mazingira ili kuepuka changamoto zote zinazotokana na Uthibiti hafifu wa Tanga nchini.

Amesema kwa mwaka huu Zaidi ya nchi 211 zimeadhimisha siku hiyo kwa lengo la kutoa elimu kwa jamii kuhakikisha mazingira yanakuwa safi na salama.

Naye Mwakilishi wa Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Segera , Mwl. Vitalis Swenya amesema wmefurahi kushirikiana na wadau hao katika kuadhimisha siku hiy,kwani ni mara ya tatu shule hiyo kushiriki katika maadhimisho hayo ikiwa ni moja ya somo kwa wanafunzi wao juu ya umuhimu wa utunzaji wa mazingira.