Na Mwandishi wetu, Timesmajira Online
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Dkt Yahaya Nawanda amewaagiza wakandarasi wanaotekeleza mradi wa Njia kuu ya kusafirisha umeme ya Msongo wa KV 220 Shinyanga(Ibadakuli) hadi Simiyu (Bariadi), pamoja na ujenzi wa kituo cha kupooza umeme cha Simiyu kukamilisha mradi huo haraka ili Wananchi waweze kuondokana na adha ya kukatika kwa umeme mara kwa mara.
Dkt.Nawanda ametoa maagizo hayo 25 Oktoba 2023 katika ziara yake katika Wilaya ya Maswa na Bariadi iliyolenga kukagua utekelezaji wa mradi huo.
“Tunataka ndani ya miezi 18 kipindi cha Mkataba mradi uwe umekamilika na utekelezaji wa mradi usiwe na mashaka mashaka na wamenihakilishia hapa kuwa kazi hii itakamilika ndani ya muda uliopangwa” alisema Mkuu wa Mkoa Dkt Nawanda.
More Stories
Watu wawili wanaodhaniwa majambazi wapigwa risasi na Polisi
Mwanasiasa mkongwe afariki Dunia
Rais Samia Kuzindua Sera Mpya ya Elimu na Mafunzo