January 23, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Wakala wa forodha watakiwa kujiepusha na vitendo vya rushwa

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Yusuph Mwenda amewataka mawakala wa forodha nchini kufanya kazi kwa weledi, uadilifu na kujiepusha na vitendo vya rushwa.

Ameyasema hayo, alipokutana na wanachama wa Chama cha Mawakala wa Forodha (TAFFA) wakiongozwa na Edward Urio Rais wa chama hicho kwa lengo la kusikiliza changamoto zao, kujadilina namna ya kuzitatua na kuboresha huduma za forodha ili kuhakisha wanalipa kodi stahiki na kwa hiyari.

Kikao hicho kilifanyika leo tarehe 01.07.2024 katika ukumbi wa mikutano wa TPA, jijini Dar es Salaam.