




Wajumbe mkutano Mkuu Maalumu CCM wakiburudika kusubiri kuzindua Ilani 2025
Na Agnes Alcardo, Timesmajira Online
WAJUMBE wa Mkutano Mkuu Maalum wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa,wakiburudika burudani ya mziki kutoka Kikundi cha Sanaa cha Tanzania One Theatre (TOT), kikiongozwa na Malkia wa Mipasho na Mziki wa Taarab, Khadija Omar Abdallah Kopa, leo Ijumaa 30 Mei 2025, jijini Dodoma.
Mkutano Mkuu Maalum wa CCM Taifa huo ukiongozwa na Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ulianza rasmi jana, 29 Mei 2025, ambao unaendelea leo katika Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete, jijini Dodoma, ambapo mojawapo ya agenda itakuwa ni kuzindua Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya Mwaka 2025 – 2030.

More Stories
TUCASA yaomba kuanzishwa sheria malipo sekta ya ujenzi
Kihongosi:Uhai wa chama mashina
Kihongosi: Msigombane kwa itikadi za vyama