Na Agnes Alcardo
KATIBU wa NEC Itikadi Uenezi na Mafunzo wa CCM Taifa, CPA. Amos Makalla, amewapongeza Wajumbe wa Mkutano Mkuu Maalum wa CCM Taifa, uliofanyika Dodoma hivi karibuni Januari 18 na 19 kwa kazi kubwa walioifanya ya kumpitisha Dkt. Samia Suluhu Hassan, kuwa mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM 2025/2030 pamoja na Kamati kuu Maalum kwa kumpitisha Dkt Hussein Mwinyi huku NEC ikimpa kura nyingi za kishindo na kuwa mgombea Urais kwa upande wa Zanzibar kupitia CCM.
CPA Makalla amesema hayo leo kwenye Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui, alipozungumza na waandishi wa habari mwanzoni kwa ziara yake ya mikoa ya kichama visiwani Zanzibar.
Amesema kuwa, kwenye Mkutano huo Mkuu Maalum Pamoja na kuwa hapakuwa na ajenda hiyo, wajumbe wa Mkutano Mkuu waliguswa na utekelezaji wa ilani iliyotekelezwa na Dkt Samia Suluhu Hassan pamoja na Dkt Hussein Mwinyi wakaona wawateue tena kuwa wagombea Urais kwa tiketi ya CCM 2025 /2030.
Akizungumzia kauli ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kuwa bila mabadiliko hakuna uchaguzi yaani ‘No reform no election’
CPA Makalla amesema suala hilo wao kama CCM haliwahusu.”Nimesikia watu wanasema no reform no election sisi wana CCM halituhusu hilo haiwezi kutokea mtu mmoja anasema hayo wana ajenda zao za siri labda kuwa hawana pesa ya Uchaguzi lakini tuna vyama 18 vilivyosajiliwa haitokuwa busara chama kimoja kije na tamko alafu wengine wamfuate. Dkt Samia Suluhu Hassan ni muumini wa maridhiano na tuna tume huru ya Uchaguzi”.
More Stories
Puma Energy Tanzania yampongeza Rais Samia kwa mazingira mazuri ya uwekezaji, yang’ara tuzo za TRA
CHAMUITA wamtunuku Tuzo Msama
‘Valentine day’kutumika kutangaza mapango ya Amboni